mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,304
- 4,793
Sasa ni mwezi wa 7 hatujawahi kupata maji ya Dawasa. Mateso tunayopata ni makubwa mno! Majirani zetu wote wanapata maji ila sisi hatuyapati hayo maji kabisa. Tangu kipindi hicho tunanunua maji tu.
Kwa sasa hatupati maji kwasababu sisi tupo eneo lenye muinuko kwa hiyo maji yahawezi kupanda huo muinuko huko yanakotoka.
Zamani tulikua tunapata maji kwasababu tulikuwa tuna line 2 za maji.. Line ya juu na line ya chini, line ya juu maji yalikuwa yanashuka mlima so tulikuwa tunayapata. Line ya chini maji yanatakiwa yapande mlima. Mafundi wa Dawasa wakatufungia hii line moja (ya juu) ambayo hii ilikuwa inatupa maji, wakabakisha line ya chini ambayo haitupi maji kabisa. Tangu hii line ya juu ifungwe imekuwa tabu mno sisi kupata maji.
Tumetoa maelezo mno lakini hatushughulikiwi.
Leo tulituma wawakilishi waende Dawasa Kinyerezi asubuhi wamekwenda lakini bahati mbaya sana hawakumkuta Manager ambae sisi tulitaka tuongee nae atupe the way forward kwa sababu hii sasa ni case study. Sio shida ya kawaida hii.
Wiki iliyopita niliahidiwa kupewa fundi, cha ajabu sana yule fundi "aliingia mitini" hakutokea na simu akawa hapokei kabisa. Hili lilitufanya tufikirie sana tukaona it's better kuonana na manager mwenyewe.
Tunateseka kwakweli. Suala sio kuelekeza maji kwetu, maji hata yakielekezwa kwetu hayatufikii, hata Jumapili iliyopita yalielekezwa kwetu ila hayafiki ndio maana nasema hii ni shida ya kubadilishiwa line tu hili ndo litakuwa msaada kwetu.
Line ya juu ambayo ilikuwa inashusha maji hii ilitufaa sana irejeshwe na Dawasa waangalie watatusaidia vipi tu.
Ahsante