Wakati watani zao Yanga sc wakiendelea kuzozana na TFF, Simba sc yatua salama Misri tayari kuwavaa Almasry CAFCC

Expensive life

JF-Expert Member
May 2, 2020
3,082
9,809
Wakuu ikumbukwe Taifa hili la Tanganyika huwa linapeleka jumla ya timu nne kwenye michuano ya kimataifa.

Caf Champions league timu mbili na Cafcc timu mbili, katika hali ya kushangaza ni timu moja pekee tu ndio imesalia kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

Kama Taifa tuna kila sababu ya kuwekeza nguvu zetu zote ili kuhakikisha timu simba sc inasonga mbele zaidi.

Hivi ninavyoandika ujumbe huu simba sc tayari imewasili mjini ismailia nchini Misri, tayari kuwavaa almasry hapo April 2 majira ya saa moja jion kwasaa za huku kwetu.

Endapo simba sc itafanikiwa kuvuka hatua hii ya robo fainali, taifa hili litaandika histori, kwani club hii kubwa nchini na Africa itapanda viwango vya vilabu Africa hadi nafasi ya tano.

C90118D4-E4A9-4EA6-8299-161E735EB81F.jpeg
 
Sema tu inafurahisha pia kuona wakati hiyo simba haina uhakika kivile wa kusonga kwenye hatua inayofuata (ya nusu fainali) kwenye hayo mashindano; mwaka mmoja tu nyuma kaka yake Yanga alicheza fainali, huku akimfunga timu mwenyeji (Mwarabu) kwenye uwanja wake wa nyumbani! Jambo ambalo hao simba hawajawahi kulifanya.
 
Ukifanya mambo kutumia akili huzaa matunda bora wacha wazozane tatizo ni kukosa elimu na kutumia nguvu...kipimo kuwa hawana akili jana walijazana uwanja wa taifa...ikabidi waziri na raisi wao washindwe kutoa msimamo!
 
Sema tu inafurahisha pia kuona wakati hiyo simba haina uhakika kivile wa kusonga kwenye hatua inayofuata (ya nusu fainali) kwenye hayo mashindano; mwaka mmoja tu nyuma kaka yake Yanga alicheza fainali, huku akimfunga timu mwenyeji (Mwarabu) kwenye uwanja wake wa nyumbani! Jambo ambalo hao simba hawajawahi kulifanya.
Mwaka huu hao warabu wakawaramba kama icecream ahmu amu amu saiv wameshamishia vita kwa TFF hasira ziishie uko
 
Mwaka huu hao warabu wakawaramba kama icecream ahmu amu amu saiv wameshamishia vita kwa TFF hasira ziishie uko
Hao Waarabu ni wale ambao walipita kwa bahati nasibu huku wakipaki basi kwa dakika zote 90 za mchezo na kujilaza hovyo uwanjani ili muda uende! Au unawaongelea Waarabu wengine!
 
Unataka Simba iwe na uhakika wa kusonga mbele wakati mechi hazijachezwa kwani unadhani huo ni sawa na mdako unaocheza na dada ako?
Sasa kama hamna uhakika wa kusonga mbele si mngesusia tu hizo mechi! Bure kabisa wewe.
 
Wanaocheza mpira wakiwa na uhakika wa kushinda ni Yanga akiwa anacheza na mawakala wa GSM.

Nje ya hapo hamna kitu kinachoitwa uhakika wa kushinda katika football.
Kumbe kile anachokisema msemaji wenu Ahmed Ally kwa mbwembwe kabla ya mchezo, ni porojo tu!
 
Sema tu inafurahisha pia kuona wakati hiyo simba haina uhakika kivile wa kusonga kwenye hatua inayofuata (ya nusu fainali) kwenye hayo mashindano; mwaka mmoja tu nyuma kaka yake Yanga alicheza fainali, huku akimfunga timu mwenyeji (Mwarabu) kwenye uwanja wake wa nyumbani! Jambo ambalo hao simba hawajawahi kulifanya.
Umeelezea vitu vingi halafu unasema simba hajawahi kufanya, hajawahi kufanya nini?
Kama kufungwa nyumbani fainali wote simba na yanga wamepigwa home fainali.
 
Wanaocheza mpira wakiwa na uhakika wa kushinda ni Yanga akiwa anacheza na mawakala wa GSM.

Nje ya hapo hamna kitu kinachoitwa uhakika wa kushinda katika football.

Wacha weee, alafu mkala nyoya..hahaha maana umeshalambwa mara 4 mfululizo hapo uhakika wa kukukanda ulikuwepo?
 
Back
Top Bottom