Wakati Tanzania tunapeleka balozi Israel, South Afrika tuliowasaidia na ukandamizwaji wanamwondoa balozi wao

Maamuzi haya yatalicost Taifa. Mwl Nyerere aliamua 'Nchi isiyofungamana na upande wowote '
Serikali hii inafanya maigizo kwa kila jambo
Ni muda tu tutaanza kuulizana kulikoni
 
Kufungamana na Israeli hakuna tofauti na kuunga mkono mauaji ya kimbari ya Rwanda. Israel is a terror state.
 
Afrika Kusini wapambane na hali yao,tuliwasaidia kupambana na ubaguzi lkn leo wabongo huko Kwao wanaonekana kama shitholes tu full kubaguliwa na kuuwawa.
Mkuu, hizo xenophobia hata Malawi ambao hawakuwasaidia wanauwawa. Kwani wanaouliwa wanauwawa na serikali au wavuta bangi ambao hata wakati tunawasaidia SA walikuwa hawajazaliwa?

Unakumbuka ile hadithi ya mbwa mwitu wa miaka kadhaa kumwambia mwana mbuzi wa miezi sita kwamba mwaka mmoja uliopita ulinitukana?
 
Itabidi wafungue ubalozi na Palestine state ku balance....mkuu

OvA
Ikiwa hivyo itakuwa sawa kabisa, kwani hata Palestine walikuwa na Mchango mkubwa kipindi cha Nyerere...Unakumbuka ndio wao waliotujengea Hospitali ya Sinza Palestina enzi hizo kama Shukran yao kwetu.?!, ni kama Msaada wa Israel na Hospitali ya Bugando kupitia kanisa.
 
Hivi nchi nyingine ambazo tuna ubalozi hazina ukandamizaji wa haki za RAIA wake?

Angalia Rwanda, Uganda, Burundi, Sudani nk haki za RAIA wao zikoje, kwanini hasira ni dhidi ya Israel tu

Mauaji kati ya warabu na wayahudi alianza Musa alipowatoa Misri, kuanzia njiani ilikuwa ni mauaji hadi wanafika Canaan, ni karne ipi wayahudi na waarabu wameishi kwa amani? Ni muda muafaka tupambane na hali zetu, ya Ngoswe...

Au we historia imeanzia 1948?
 
 
Wavuta bangi sio?Julius Malema nae ni mvuta bangi sio?au hua huoni akihamasisha kuua/kufukuza wageni nchini kwao.

Watu wa Afrika Kusini ni MBWA KABISAA wala hawana maana yoyote ile,pole zangu za dhati kwa Palestina kwa wanyopitia lkn sina haja ya kuungana na South Africa kwa chochote kile.
 
Ndugu ubalozi wetu upo Palestina siku nyingi!
Tanzania does not currently have any diplomatic or consular representation in Palestine kaka ila wao wana ubalozi wao hapa 1/9 Chisiza Close Oysterbay
 
Acha kulinganisha Taifa lenye akili, maono na mwelekeo chanya (Tanzania-isiyopenda vurugu na ugaidi) na taifa la kishenzi lenye kusahau mchango wa wengine katika kupigania uhuru na kuondoa baguzi wa rangi(South Afrika).
Kumbuka kuwa hawa waisraeli walikuwa wanaunga mkono Serikali ya kibaguzi ya Afrika kusini enzi hizo SA ilivyokuwa imetengwa na Dunia
 
Maamuzi haya yatalicost Taifa. Mwl Nyerere aliamua 'Nchi isiyofungamana na upande wowote '
Serikali hii inafanya maigizo kwa kila jambo
Ni muda tu tutaanza kuulizana kulikoni
Naamini unafahamu kuwa hata waarabu wana ubalozi na Israel, mojawapo ni Saudi Arabia, ni kipi kinakufanya uichukie Israel kuliko waarabu wenyewe?
 
Hivi waisrael kwao ni wapi?
Hahaha! Mkuu swali fupi lakini lilisumbua sana vichwa vya UN mwaka 1948. Lina historia ndefu sana. Ni kwamba, Israel, walipokuwa utumwani Misri, walipewa eneo la Palestina na Mungu kama nchi ya ahadi. Hivyo waliongozwa na Musa na baadae Joshua kutoka Misri hadi nchi ya Palestina, ambapo waliwakuta Wafilisti (ambao inaonekana ndio Wapelestina wa leo). Waliwashinda vita wakachukua lile eneo la Israel, japo kulikuwa na ugomvi kila siku, kina Daudi na Goliath, Samson wa Delila nk.

Sasa mwaka 70 AD, miaka kama 40 baada ya Yesu kuuawa, nchi ya Israel ilipigwa vibaya na Waroma. Kumbuka wakati Yesu anauawa Israel ilikuwa chini ya utawala wa Roma. Israel walianza uasi ambao kikomo chake kilikuja mwaka 70, ambapo Waroma waliwaua karibu Israel wote na kuvunjavuna na kuchoma moto lile hekalu Yesu alipokuwa akihubiri. (Kumbuka Yesu alitabiri kuwa halingesalia jiwe juu ya jiwe kwenye lile hekalu, na ndicho Waroma walifanya). Waisrael wote waliobaki walipelekwa utumwani katika himaya ya Roma ambayo wakati huo ilitawala dunia nzima. Sasa kuanzia mwaka huo 70 Israel ikawa haipo tena ile nchi ya ahadi. Sasa kumbuka kulikuwa na Wafilisti jirani (Wapalestina) ambao walirudi kuchukua tena eneo lote la Israel baada ya Israel kupigwa na kuondolewa kwenda Roma.

Sasa miaka mingi baadae Israel walitawanyika sehemu mbalimbali duniani toka huo mwaka 70, wengine wakawa Germany, Marekani nk. Sasa wakiwa wametawanyika, walinyanyaswa na kubaguliwa sana, kwa kuwa walionwa kuwa wauaji wa Yesu. Marekani walibaguliwa sana, hata univerity kama Yale likuwa marufuku kwa Waisrael kwenda (jews). Kumbuka Israel kwa ujumla hawamwani Yesu, wanasema yule alieuawa hakuwa Yesu Masihi, hivyo hadi leo wanasubiri Masihi aje. Mateso waliyopata toka kwa Hitler ilifanya Umoja wa Mataifa uanze kutafakari kuwatafutia nchi yao. Hata ilipendekezwa waletwe hapa Uganda, ili Uganda iliyokuwa chini ya Uingereza wakati huo ndio iwe nchi yao. Ndipo Israel wakasema kwamba, tukisoma Biblia, mbona sie tuna nchi yetu, Israel (wakati huo haiitwi Israel). Tatizo ikawa kwamba, watawarudishaje Israel wakati waliondoka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na ile nchi sasa inakaliwa na Wapalestina? Watawapeleka wapi Wapelestina ili Israel wapewe ile nchi?

Ndipo mwaka 1948 uamuzi ukafanyika kwamba basi ile nchi igawanywe katikati (hata Jerusalemu igawanywe katikati), nusu wapewe Israel, na nusu wapewe Palestina. Ile nusu ya pili ndio ikaitwa tena Israel.

Sasa Palestina na waarabu wengine hawakufurahia huu uamuzi. Kwa muda mrefu wakawa wanawashambulia Waisrael. Baadaye, miaka ya 1970 hivi, Israel waliweza kujibu mapigo wakachukua hata ile sehemu ambayo Palestina walipewa, pamoja na sehemu ya Syria (Milima ya Golan) ambao walikuwa wakiwasaidia Wapalestina, na wakasema kuanzia wakati huo watazikalia sehemu walizoteka kimabavu na hawatazirudisha tena kwa Palestina au Syria. Wakaanza kujenga nyumba zao za kuishi kwenye maeneo yanayoitwa "occupied territories". Pia wakachukua sehemu yote ya Jerusalem, hata waliyopewa Wapalestina. Wakawaachia Wapalestina sehemu ndogo sana, Gaza.

Sasa huo ndio ugomvi uliopo. Palestina wanadai warudishiwe eneo lao, na baadhi yao hata bado wanaona haikuwa sahihi nchi yao kugawanywa katikati ili wapewe Israel. Israel wanasema tulishinda vita hivyo hili ni eneo letu kihalali.

Sasa watu kama kina Nyerere, walikuwa na msimamo kwamba pamoja na kwamba ilikuwa vita, si halali Israel kuendelea kukalia eneo la Palestina na Syria kimabavu. Hivyo walisema ni vema Israel warudi kwenye eno walilopewa na Umoja wa Mataifa. Wanasema lazima kuwe na two states, huku Jerusalem imegawanywa katikati. Israel hawataki.

Ni sawa na Tanzania tungekalia Uganda kimabavu kwa kuwa tulishinda vita na kuingia Uganda yote!

Lakini ugomvi wa Palestina na Israel ni wa tangu enzi za Daudi na Goliath, ndio maana kwa baadhi ya watu wanaona kwa sababu za kidini wawe upande wa Israel wakiona ni upande wa Mungu!
 

Hili sio suala la dini wa ukabila, kwanza hua tunakosea tunapoyachanganya mataifa, uarabu ni sawa NA Ubuntu uliotapaka Karibia African nzima.

Hao waarabu wauza petroli leo wana msimamo mmoja na waisraeli na wamerakani.

Kama watanzania tunajulikana kwa utetezi wa haki za binadamu.

Tusiyachanganye yasiyo changanyika
 
Umeeleza vizuri lakini umeshindwa kueleza kabla hawajaenda utumwani Misri nchi yao ni ipi. Hivyo fafanua hapo ili kuweka records sawa boss.
 
Mkuu naona unaleta dini. Mie ni Mkristo, naamini hakuna kukombolewa pasipo kupitia kwa Yesu. Sasa siamini kwamba kupitia kwa Israel kama taifa ambalo sio la Kikristo, tunaweza kupata baraka.
Soma tena Biblia,
Kama unajifanya mkristo mbona umekua kipofu, kwani wana Israel wa saizi wamebadilika wamekua tofauti na wale wa kipindi cha Musa?
Mana kipindi cha Musa Mungu ambaye ni NIKO AMBAYE NIKO aliwaongoza hao hao wana Israel kipindi hicho kwa kuwapiga adui za Israel ili wafike Kanani, au unafikili Mungu aliwaondoa kwa kutokupigana?
Mungu huyu huyu ndiye aliyesema atawatawanya na kuwa watumwa na kisha kwa sababu ya kukumbuka agano lake na Ibrahim alisema atawakusanya tena,
Ko msitegemee Mungu atawakusanya tu hivi hivi Bali kama walivyokua anawaleta kutoka Misri.
Issue ya Tanzania sidhani kama kuna umuhimu wowote wa Tanzania kuanza kujigiza kwenye ugomvi wa mataifa mengine, Tanzania lazima hiangalie maslahi yake kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…