TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,578
Habari wadau.!
Wakati Tz na Kenya wao mambo yao yanalega lega na kupinda pinda huku mama akipambana kuyanyoosha wao waganda wapo mbioni ku launch kinu cha nyuklia kwa "mpango wa amani" ambapo nuklia hiyo itazalisha takribani 41,700Megawatts mpaka kufikia 2040.
Uganda wameingia mkataba na wachina ambao watasanifu, watajenga na kuendesha mradi wa nyuklia,hii inafanya Uganda kuwa nchi ya pili kwa Afrika kwa uzalishaji wa umeme kupitia nyuklia ukiachia mbali SA ambayo ni ya kwanza.
Tukumbuke pia waganda hawa hawa wana mafuta ghafi ambayo yatasafirishwa kuja Tanzania,inaonyesha waganda wamejipanga sana kuliko hata nchi nzingine.
Tanzania sio kwamba hatuna haya madini ya nyuklia ,yapo mengi sana kule kwa kina Komba kule Namtumbo Ruvuma pia yapo maeneo kama Namtumbo (Mkuju), Bahi, Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
Hizi ni fursa ambazo serikali na wizara inabidi iwalete wawekezaji waje kuwekeza kwenye hii "Mkuju River Project "waache kusuasua na sisi twende kwenye huo umeme wa nyuklia ,pia nyuklia ina matumizi mengi hata mahospitalini n.k japo tuna bwawa la Nyerere ila mahitaji ya umeme yanaweza yakawa makubwa sana siku za usoni.
Pia miradi kama hii itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wetu ,swala kama hili linatakiwa wizara ya madini kufanya fasta kuakikisha maeneo yenye deposit yanapata wawekezaji haraka sana ili kazi iendelee.