Wakati mwingine wanasiasa wawe wakweli, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa hakuwa na ziara rasmi Tanzania

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866



Naona watu wameibeba hii ya Katibu Mkuu wa UN kama "ajenda" tena,huku namuona Mtatiro akirusha makombora,na huku Mbunge Msigwa akirusha kwa upande wa pili.Vijana nao wamebeba mitandaoni kama ajenda ya kumalizia week kimjadala.

Watu wanatakiwa kuelewa tu,mambo mengine sio lazima tuingize siasa saaaanaa.António Guterres hakuwa na ratiba ya ziara ya Tanzania.Ziara yake ilipangwa kufanyika Somalia ili kuonana na Rais mpya kuhusu baa la njaa na ukame unaolikumba eneo hilo.

Sehemu ya pili ikawa Kenya kukutana na Kenyatta,na hii ni kwa sababu,nchini Kenya kuna kambi kubwa sana ya wakimbizi ya Dadaab, inayokaliwa na Wasomali,ambao sera ya Trump ya katazo la Wasomali kuingia US imewaathiri...Umoja wa Mataifa lazima iwahikikishie Kenya ushirikiano ktk kipindi hiki cha mabadiliko ya sera za uhamiaji nchini Marekani.

Maana hivi karibuni,wakimbizi wengi wenye asili ya Somalia ambao walikuwa wafanyiwe "resettlement" na Shirika la Wahamiaji la Kimataifa (IMO),kutoka kambi ya Dadaab kwenda Marekani wamezuiliwa kutokana na sera mpya ya Marekani,hivyo kuwafanya waendelee kusalia Kenya.

Hapa Tanzania alikuwa tu "On Transit",sababu ndege aliyotumia kusafiri ni SwissAir.Schedule ya SwissAir ni Zurich-Nairobi-Dar-Zurich.Na inapotoka Nairobi kuja Dsm kabla ya kwenda Zurich,ndege huwa inakaa Dsm zaidi ya saa moja na nusu.Sasa mtu mkubwa kama Antonio hawezi kukaa muda wote huo ktk ndege wakati anaweza kushuka na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi wa Tz kama wadau wa Umoja wa Mataifa.

Aina hii ya ugeni ni ya kawaida sana katika viwanja vya ndege ambayo hutumika kama "connection centre".Ukienda Jomo Kenyata International Airport VIP Lounge utakutana na Marais wengi na viongozi wengi maarufu wakipiga soga na Mawaziri wa Mashauriano ya Kigeni wakati wakiwa "on transit".Bole International Airport pale Addis Ababa VIP-Lounge humkuti Waziri Mkuu wa Ethiopia,lakini toka mawio mpaka machweo ya jua,viongozi wa kimataifa huwa "On Transit" kuelekea katika safari zao tarajiwa.

Hata kwa kumtazama tu,wale waliowahi kupanda SwissAir First Class,watakubaliana kuwa alichokuwa amekivaa Guterres ni zile pyjamas (pajama) za abiria wa daraja la kwanza ambao hupatiwa ndani ya ndege kwa ajili ya kupumzikia kwa safari ndefu.Dressing code tu ya pyjamas za SwissAir zinaashiria Katibu Mkuu alikuwa "On Transit".Ratiba na Tanzania haikuwepo.

Sio wa kwanza Guterres kupita tu bila kuonana na Rais,wapo viongozi wengi hupita kama "On transit" hapa Dsm,na husalimiana na viongozi wa chini wa serikali.Mfano King Mswati,yeye "refueling point" yake huwa ni Dsm,katika safari zake za kutoka Mbabane kwenda ama Abu Dhabi shopping au sehemu nyingine,kituo chake cha Cattering na refueling ni Dsm.Toka enzi za JK mpaka sasa,huwezi kumkuta JK anakimbizana kumpokea Mswati,bali utamkuta Membe kwa minajili ya kidiplomasia akimsubiri King Mswati.

Uwanja wetu wa Dsm hutumika kwa ajili ya "On Transit Passengers" na "On Transfer Passengers"."On Transit Passengers" ni wale abiria ambao hupita uwanjani wakiwa ndani ya ndege bila kushuka na kuchukua abiria wengine au kushusha na kuunganisha na ndege hiyohiyo kuelekea "destination" iliyokusudiwa.Mfano wa ndege zenye safari ya aina hii Julius Nyerere Int'nal Airport ni SwissAir (Zurich-Nairobi-Dsm-Zurich),Ethiopia Airways (Addis Ababa-Dsm-Znz au Addis-Dsm-Hahaya Comoro),Oman Air (Muscat-Znz-Dsm-Muscat),Mauritius Air nk.

Siku kadhaa kiongozi wa Mauritius alipita Dsm na Mauritius Air na kuunganisha kuelekea Addis Ababa kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika.Toka Sir Seewoosagur Ramgoolam Port Louis kupitia Julius Nyerere International Airport mpaka Addis Ababa.

Walikutana tu na Rais wetu ndani ya ndege,wakapeana mkono na kila mtu akarudi kwenye presidential Suit room yake ya "First class".

Hii ni dalili ya uwanja wetu kukua na kuanza kuwa moja ya "Connection" kubwa ya sehemu mbalimbali za Afrika na dunia.Sasa tunapokea abiria wote wa kutoka Msumbiji kwenda Dubai kupitia Dsm,abiria wa Mayote na Comoro kwenda Dubai.Abiria wa kutoka Mauritius kuja Afrika ya Mashariki na Mashariki ya kati ya Asia.

Tuanze kuzoea,kuwa sio kila abiria ni "mgeni rasmi" wa nchi,wengine wanakuwa wapita njia.Waziri Mkuu wa Ethiopia angekuwa anashinda Airport kama kila kiongozi anayepita Bole Int'nal Airport atamsubiri kumpokea.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm angekuwa anajipanga kila siku kupokea viongozi na mawaziri mkoani kwake,maana ofisi zote kubwa zipo kwake.Waziri wa Mambo ya ndani akiwa Simiyu ni "mgeni",ila kwenye viunga vya Dsm ni mpita njia tu.

Hence;haikuwa sehemu ya ratiba,ndio maana ni Balozi Mahiga badala ya Rais JPM
 
Unaangalia hali yako na uzito wa mgeni husika kisha unajiongeza.Kama vipi hata huyo waziri hakuwaa na sababu ya kwenda.

Nina uhakika angekuwa ni Kikwete hata Ikulu angemkaribisha japo ni kwa muda mfupi au angeenda Airport kumuona.

Angekuwa ni Trump katua kwasababu yoyote ile Magu asingeomba kukutananae?
 
Msigwa bado hajaamini kuwa ameteuliwa pale ikulu akijua hakustahili kuwepo pale amebebwa tuuu
 
Hongera sana mkuu wamezoea kukosoa kila kitu wakati kuna vitu hawavijui au wamezoea kupindisha ili wapate umaarufu wa kisiasa.Narudia tena hongera sana umetupatia somo zuri,na sijui kama wataonekana kwenye huu uzi.
 
Ufafanuzi mzuri sana...ubarikiwe
 
Magufail hakuwa na ujasiri huo wa kukutana na katibu mkuu.
Afadhali ingekuwa rasmi ina maana kungekuwa na agenda, sasa hakuna agenda angeanzaje ku derive agenda ukizingatia kiinglish ni bashite???!!!

Anachoweza ni kujipeleka kwa pengo kupanga mikakati, laki kwa wakubwa wa dunia hii anajificha idodyandole.
 

Magufuli angeenda kuonana naye Airport sasa hivi mngekuwa mnamsema. Chadema hana jema!
 
Hivi nyie mnatetea hata jambo lililo wazi kabisa, ni kwamba hata kama alikuwa anapita kwakuwa amechagua kutua TZ kabla ya kuendelea, protoko ilitakiwa izingatiwe.Mfano mdogo raisi Magufuli akiamua kwenda Dodoma kwa gari afikapo Moro lazima apokelewe kiprotoko kisha aagwe kuendelea na msafara.Vivyo hivyo kama anakwenda Mwanza kwa ndege ambayo ratiba yake ni kutua Tabora kwanza kabla ya kuendelea na safari lazima uongozi wa tabora protocally umpokee na kutumia nafasi hiyo finyu kueleza kitu fulani kwa raisi chenye manufaa kwa mkoa
 
Kwa hoja yako,basi Ethiopia watu wangekuwa wanashinda Airport kusubilia kila kiongozi anayepita!!Hizo ziara za Magufuli zinakuwa ni rasmi,hii ilikuwa ni "On Transit".

Zingatia hili neno "On Transit"....Ndio maana hata taratibu za uhamiji na Forodha hazikufuatwa,sbb huyu mtu hakuwa rasmi,alikuwa anapita tu,aibu ingekuwa amepita bila hata Waziri wa Mashauriano ya kigeni kumsalimu.

Sio kila jambo tunalitafutia upande wa pili wa kukosoa.
 
Mara ngapi raisi amesimamishwa njiani akiwa anaelekea mahala kwenye ziara na akaongea hata kutatua kero za wananchi??
 
Hata Mimi nilituaga Kenya nikabadilisha ndege mbona akaja waziri tukasalimiana zen nikaendelea na safari yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…