Wakati hofu kuhusu akili bandia ikitanda Afrika, China na Afrika zinaweza kufanya nini pamoja?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,099
1,095


Kutoka kilimo hadi matibabu, akili bandia inabadilisha kila nyanja ya maisha ya binadamu. Hata hivyo, barani Afrika, watu wana maoni tofauti kuhusu akili bandia, na hata hofu ni kubwa zaidi kuliko matarajio.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Mfuko wa Lloyd’s Register ambao makao yake makuu yapo mjini London, ni 13% tu ya watu katika Asia Mashariki ambao wanaona kuwa akili bandia ni wazo baya, na karibu 60% ya waliohojiwa wanaipokea sana, mtazamo kama huo pia unabebwa na watu wa Ulaya.

Eneo lenye mashaka zaidi kuhusu akili bandia ni Afrika Mashariki, ambako katika nchi kama Tanzania, Kenya na Uganda, zaidi ya nusu ya waliohojiwa wanaamini kuwa teknolojia ya akili bandia inaweza kusababisha madhara.

Lakini hali halisi ni kuwa sekta mbalimbali barani Afrika tayari zimeona manufaa ya akili bandia. Katika sekta ya kilimo, Afrika tayari inatumia zana zinazoendeshwa na akili bandia kuchanganua mvua na hali ya udongo na kutoa mashauri yanayotekelezeka kwa wakati, ili kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa kilimo mashambani.

Katika huduma za afya, akili bandia tayari imetumiwa kuwasaidia madaktari kufuatilia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza ili kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa kama vile malaria, kifua kikuu, na kuhara. Na katika benki, teknolojia ya akili bandia inatumiwa kutathmini hali ya biashara ya kampuni ndogo ndogo na kutumia vizuri taarifa hizi kutoa mikopo, na kuleta mabadiliko katika uchumi halisi na kadhalika.

Kwa mtazamo huu, suluhu za akili bandia zina maana kubwa katika bara la Afrika, lakini ukosefu wa fedha kimataifa na uandaaji wa wataalam imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya akili bandia barani Afrika.

Kutumia nguvu mpya za uzalishaji kuhimiza maendeleo ya taifa ni matokeo muhimu yaliyofikiwa kwenye Mikutano Miwili ya China ya mwaka huu, na kwamba China inaongeza nguvu za uvumbuzi, kulima na kupanua viwanda vinavyoibukia, na kupanga mapema viwanda vya baadaye. Kwa kutumia sayansi, teknolojia na uvumbuzi, mamia ya mamilioni ya watu nchini China wameondokana na umaskini, na China imekuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani. Hivi sasa China inaunganisha mwelekeo huu mpya wa maendeleo ya kiuchumi katika pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ili kukuza ustawi wa pamoja kwa binadamu.

Afrika itakuwa mnufaika mkubwa wa maendeleo ya China ya nguvu mpya za uzalishaji na kusaidia kutatua changamoto za ukosefu wa ajira, umaskini na ukosefu wa usawa. Katika Kongamano la Maendeleo na Ushirikiano wa Mtandao wa Internet la China na Afrika lililofanyika hivi karibuni, China na Afrika kwa pamoja zilitoa tamko la mwenyekeiti kuhusu ushirikiano katika nyanja mpya za kiteknolojia kama vile akili bandia.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, maendeleo na matumizi ya taarifa za akili bandia yana umuhimu mkubwa kwa nchi nyingi zinazoendelea zikiwemo China na nchi za Afrika.

Manufaa ya akili bandia kwa Afrika yatazidi yale ya bara jingine lolote duniani, na kwamba dhana mpya za maendeleo ya China ya kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zinaendana sana na mahitaji ya sasa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Afrika, pamoja na mikakati na maono ya maendeleo katika siku zijazo, hivyo akili bandia italeta fursa mpya na msukumo mpya kwa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Inaaminika kuwa akili bandia itakuwa mada muhimu katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika Beijing mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…