tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,491
Wakati katika jiji la Dar es salaam vyombo vya dola vinahangaika kuhakikisha kabisa kuwa vijana wanaojiita 'Panya road' wanatokomezwa kabisa ambao ni maarufu sana maeneo ya Yombo,Buza na baadhi ya maeneo ya Mbagala na Mburahati basi Mkao wa Mbeya ambao inasadikika kuwa una rais wao waliemchagua ili kuwaongoza limeibuka kundi la 'Wakorea weusi' lenye malengo kama Panya road wa Dar linalotishia wakazi wa jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa kuwapora mali na kuwajeruhi kwa kuwavizia nyakati za jioni.
Akiongea na baadhi ya waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamanda Mohammed Mpinga alisema 'kuna kikundi cha vibaka waliojiita Wakorea na tayari walishatiwa mbaroni tangu Desemba na kesi yao ipo mahakamani na baada ya mahojiano tulibaini ni wavuta bangi ila hao wanaojiita Wakorea weusi inaweza ni kikundi kingine lakini tunaendelea na kuimarisha ulinzi kwa kufanya doria muda wote'
Hivi karibuni Afisa masoko wa gazeti la Mwanainchi alivamiwa na kikundi hicho karibu na nyumabani kwake akitokea kazini kwa kupigwa na kuporwa simu na fedha.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Makunguru Emiliana Siulanga anasema kutokana na tishio hilo mtaani kwake wameanzisha ulinzi wa jadi mfano wa sungusungu na imesaidia vikundi hivyo kufanya uhalifu.
Lakini tatizo kubwa la vikundi hivyo kutimiza uhalifu huo ni kuwa wanainchi wanawaficha vijana hawa na kutotoa ushirikiano kwa viongozi wa mitaa na si kwamba vijana hao hawafahamiki ila shida kubwa ni kulindana kwa misingi ya ukabila.Kijana akikamatwa basi wazee wanaibuka kumtetea kuwa huyu ni wa nyumbani kwa maana makabila ya hapo Mbeya.
Nadhani rais wa Mbeya na viongozi wa usalama pamoja na jamii kwa ujumla mna kazi ya kufanya ili vikundi hivi visambaratishwe kabisa kama ilivyo Dar kwa sasa husiki kuhusu panya road.