Wakamatwa baada ya kukutwa wanakunywa bia Alfajiri Coco beach

Alure

JF-Expert Member
Dec 27, 2014
1,100
1,053
Dar es Salaam: Hii ni baada ya tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza kufungwa kwa Bar zote ifikapo saa sita usiku ‘Tumewakuta watu hawa katika maeneo ya Coco Beach alfajiri ya leo wakiwa wanakunywa pombe mida hiyo, naomba hii iwe ni fundisho kwa watu na serikali imeshakataza watu kukesha Bar'

Maoni yangu:
Sasa naona huku tunapoelekea sio,yani had Pesa yangu naamuliwa muda Wa mwisho kuitumia.
 
mbona huo mchezo Coco beach wanaucheza sana, yani hapo ndo wanapoponea. usikute hao jamaa waliombwa mali ya mfuko wakajifanya wagumu ndo wakalikwaa hilo, na kuna wengine wanabambikiwa kesi za kungonoka hadharani hapo hapo coco beach. polisi wa kule ni nyoko
 
Mnaweza ona ni serekali ya kijamii kumbe kuna pembe moja inaamrisha yote yafanyike bila kuzingatia collective responsibility sioni mbinu mikakati juu ya jambo flani kwa wanaohusika na jukumu ilo ila utasikia kwa "awamu hii, kwa kuzingatia kauli ya mbiu ya Mh...., etc
 
Kijana acha kukurupukaeti kwa kuwa ni fedha yako basi ufanye mambo yako pasipo fuata sheria,pia pendeni kusoma mambo ya maana kabla ya kuanza kuloloma tu,je kuna sheria inayokataza watu kulewa asubuhi,jiulize na ukipata jibu ndio uanze ''kudai uhuru'' wako tatizo nikuwa nchi watu tulishazoea kufanya mambo kienyeji bila kufuata taratibu sasa tukikumbushwa huanza kulalamika,kila nchi ina desturi,tamaduni zake na sheria zake.Uhuru ukivuka mpaka mwishowe huwa madhara.
 
Haya ww unaejua hzo sheria,tutajie hyo sheria inayosema hatakiwi mtu kunywa bia muda anaotaka yy na inapoonyesha kuwa muda wa kunywa bia ni kuanzia muda fulani had fulani .....
 
Bila pombe hiii nchi msahau barabara nzuri,hospitali,madaraja nk! Ni aibu kwa kweli manake madini,gesi,utaliii,viwanda vimewashinda kilichobaki nikuongeza tu kodi kwy pombe na sigara.
 
Sasa ninutajiri kwa wauza gongo,maana vilinge vya gongo vipo mafichoni au vipi?,serekali iandae bajeti ziada ya afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…