Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,508
3,992
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.

Kikwete Azungumza na Wajumbe Kuhusu Rais Samia Kugombea Urais 2025

"Azimio liwe Rais Samia amechaguliwa kuwa mgombea Rais wa CCM 2025"

Rais mstaafu na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete, alilazimika kutoa busara zake baada ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM kutaka kuanzisha mjadala kuhusu wagombea wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kupitia chama hicho.

Katika kikao hicho, ilikubalika kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, pia akijitokeza kama mgombea mwenye nguvu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu wa kihistoria unaonyesha imani kubwa na matumaini makubwa ambayo CCM inayo kwa uongozi thabiti na wa kimkakati wa Rais Samia, pamoja na dhamira yake isiyotetereka ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi, ujenzi wa miundombinu, maboresho ya huduma za afya, na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya "4Rs. Akiwa Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania, Rais Samia si tu kwamba amevunja vikwazo vya kijinsia, bali pia ameweka viwango vipya vya uongozi shirikishi na wa maono.
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amesema Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM wamalize kazi leo leo ya kumpitisha Rais Dkt. Samia Suluhu kuwa mgombea wa Urais wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kugombea Urais wa Zanzibar Urais 2025
View attachment 3206168
Hii hoja itakuwa ilikuwepo kwa kificho na walikuwa wamempanga mtu wa kuitoa! Hii yote ni kutokana na ukata wa kuitisha mkutano mkuu mwingine, fedha yote imeishia kununua Yu Tong!
 
Kikwete ameipangua hoja hiyo kwa akili sana.

"Mwali hatolewi nje mpk siku 30 ziishe"

Kasema wasifanye uamuzi unaokinzana na sheria, kanuni na taratibu za nchi
Naona JK kama kaingia Ubaridi ivi
Kikwete ameipangua hoja hiyo kwa akili sana.

"Mwali hatolewi nje mpk siku 30 ziishe"

Kasema wasifanye uamuzi unaokinzana na sheria, kanuni na taratibu za nchI
 
Back
Top Bottom