Wengi wetu sio wageni kuziona video za wakristo wanatemewa mate wakienda Israel, Ni matukio yanayotokea mara chache lakini kwa jinisi yanavyotrend yanajenga picha kwamba ni matukio ya kila siku na wayahudi wote wapo hivyo, LA HASHA !! Ni jamii ya wayahudi wa Heredi, Kwa idadi yao kuna myahudi wa Haredi moja katika kila wayahudi 10.
Wanakupinga uwepo wa taifa la Israel – Ukiona kuna maandamano ya kuipinga Israel basi si ajabu kuwakuta waisrael wamevalia mavazi meusi wamebeba bendera zenye maneno kama "Israel ifutwe", Ajabu ni kwamba wao wanaishi Israel hawataki kwenda nchi zingine.
Hawataki kwenda jeshini – Wayahudi wa Heredi ni mwiko kwao kwenda jeshini, ni kwasababu kwenda jeshini ni kusapoti uwepo wa Israel na kuilinda Israel, Ajabu ni kwamba Israel ikishambuliwa na makombora huwa wanaomba kulindwa na jeshi la Israel.
Hujitenga na wayahudi wengine – hawapendi muingiliano na jamii zingine, wanaishi kwenye mitaa / vijiji vyao, hawataki kuoana na wayahudi au jamii zingine, wana shule zao maalum, n.k.
Hutemea mate wakristo – Ukienda Israel ukikutana na Myahudi wa Heredi akikuona umevaa msalaba ama umeshika biblia tegemea kutemewa mate
Upekee wa kimavazi – Hupendelea kubaa makoti meusi, mashati meupe, kofia nyeusi na kufuga ndevu.
Uchumi – Hutegemea zaidi misaada ya serikali, pesa za vikundi, charities, n.k.
Dini – Wao kwenye dini wapo very extreme tofuti na wayahudi wengine, wao huona dini nyingine ni takataka, Elimu inatakiwa iwe ya dini zaidi kuliko elimu dunia, wanataka serikali ya dini, n.k.