Wajua, kuna 2 Types of Leaders. Born Leaders na Manmade Leaders? Je, Wajua tutamfaidi zaidi Rais Samia kipindi cha 2025-2030 kuliko sasa If Only?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,279
120,689
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo makala yangu ni makala ya dhana dhanifu, kuhusu Tanzania ya 2025 -2030.

Makala ya leo kwanza inafundisha kujua types mbili za leaders, kuna born leaders, na made leaders, na kwenye made leaders kuna manmade leaders na selfmade leaders. Na ndani ya makundi hayo makubwa mawili pia kuna sub groups za leaders ambao ni leaders leaders na leaders ambao ni technocrats leaders.

Kwa vile kwa sasa rais wetu ni Rais Samia, hivyo nashauri tuanze na Samia Ili kupata Viongozi Bora baadae, Watanzania tujifunze kuwasoma watu kwa asili zao. Mjue Samia alivyo kwa asili yake

Je wajua kuwa licha ya Tanzania na Watanzania kumfaidi Rais Samia kwa makubwa anayoyafanya sasa, japo Rais Samia ni born leader yaani God made leader lakini ameupata uongozi kwa manmade kwa kushikwa mkono na watu, kwa jina lake kupendekezwa na watu, kuwa VP, na ndipo hatimaye kuupata urais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu, hivyo kama sasa tuu hivi alivyo ni rais kwa kudra tuu, amefanya makubwa haya anayoyafanya na anaendelea kuyafanya mambo makubwa mazuri ya kupendeza ya neema na mafanikio, can you imagine 2025 - 2030 tutakapokuwa tumempa rasmi, kwa kumchagua kupitia sanduku la kura, itakuwaje?.

Sii wengi wanajua kuwa japo sasa tutamfaidi sana Rais Samia, lakini tutamfaidi zaidi na zaidi iwapo Rais Samia ataendelea na urais wa 2025 - 2030, kuliko sasa?. Ni kwanini,
Andamama nami!.

Naomba kabla ya kusoma bandiko hili, umezuka mtindo mtu yoyote akimpongeza kiongozi yoyote, ananyooshewa vidole vya uchawa!. Hili sio bandiko la uchawa wala mimi sio chawa wa Mama wala chawa wa mtu yoyote na hili nimelisema wazi Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na hoja ya mwana JF huyu
Wengi tunatamani mama sasa asimame mwenyewe tumuamini badala ya imani iliyopo kuwa kuna mtu anaongoza kwa remote. Akibadili baraza abadili na utendaji wake kama bado anayonia ya kuwania Urais 2025.
Mkuu MTAZAMO , kwanza niendelee kukupongeza wewe ni miongoni mwa wana JF very objective.

Kuna viongozi wanasiasa wa aina mbili, born leaders na made leaders na sub groups mbili.
1. Born leaders who are responsible to the people!.
2. Made leaders who are (a)manmade leaders who are responsible to those who made them!.
(b) Self Made Leaders who are not politician leaders but technocrats, who are responsible only to themselves!.

1. Born leaders, ni viongozi wanaozaliwa na karama ya uongozi, ambao ni leaders responsible to the people, hawa ni wale viongozi wanasiasa waliozaliwa na kipaji cha uongozi kwa wito wa utumishi wa watu, hawa ni selfless leaders ambao kwao ni taifa kwanza, na wameutafuta uongozi kwa juhudi zao wenyewe binafsi kihalali bila kubwebwa na mtu au kutumia rushwa au ukwasi wao kununua uongozi, hivyo wanawajibika kwa watu, na hawawajibiki kulipa hisani kwa yeyote!. Hawa ni viongozi kama Nyerere, Karume Snr, Jumbe, Kawawa, Mkapa na wengine, they are born leaders, wameutafuta uongozi kwa juhudi zao binafsi bila kubwebwa na yeyote au kutumia rushwa, hivyo they were indebted to no one!, na wanaongoza kwa mifano.

Naomba kuliruka kundi la pili la
born leaders ambao pia ni Made leaders na kurukia kundi la Self Made Leaders who are technocrats, are responsible only to themselves!, kwenye kundi hili ndio kuna Magufuli, huyo ni self made leader ambaye alikuwa a technocrat ndio maana aliongoza kwa mtindo wa nyapara style ya mkono wa chuma na hakuwa indebted kulipa fadhila kwa yeyote ndio maana alitawala as if he own this country ni mali yake na anaweza kufanya lolote na chochote na hakuna wa kumuuliza.

Sasa nirudi kwa kundi la pili la
2. Made leaders , kwenye kundi hili pia kuna born leaders ambao wameminywa na kunyimwa fursa, hivyo mpaka watokee watu wawashike mkono, wawanyanyue na kuinuka, who are leaders who are responsible not only to people, but also to those who made them!. Kundi hili lina Mwinyi Snr, Karume Jnr, JK, Mwinyi Jnr na Samia. Unaweza kuangalia Samia aliishaonyesha uwezo siku nyingi sana angalia toka lini tumemtaja New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!

Na wakati tukiangazia sifa za Mwanamke kuweza kuwa rais wa Tanzania, jina la Samia Suluhu Hassan liliibuka kinara Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?

Japo they are born leaders, but they had to be made leaders hivyo they are not only responsible for the people, but indebted to those who made them, who they are hivyo kuwa ni watu wa shukrani!, hivyo wale mnaopiga kelele mara muondoe huyu, mara muondoe yule!, mtapiga sana kelele za mlango, ama kama kelele za chura kisimani!.

Japo ni kweli baada ya Rais Samia kuupata urais kwa kudra tuu za Mwnyeenzi Mungu, Rais Samia angependa kuona Watanzania wakichagua rais Mwanamke na yeye ana nia ya dhati ya kuwania urais 2025 ila ana changamoto Kuu mbili.

Changamoto ya kwanza ni jee ni yeye aliyepangiwa na YEYE kwa 2025?. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Changamoto ya pili ni HII sauti !.

Awamu hii ya kwanza ndio awamu pekee ya kudra, hisani na fadhila, Watanzania tukimchagua Rais Samia kwa awamu ya pili, hii sasa itakuwa ni awamu yake ya self made leader, besides being a born leader, atakuwa hawajibiki kulipa fadhila kwa yeyote na hapo sasa ndio Tanzania na Watanzania tutamfaidi vizuri zaidi the real Samia I know, ambaye ni Samia huyu niliyemzungumza hapa! Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

Ila sasa kufuatia possibility ya ile changamoto ya pili kuja kuwa kweli, naendelea kumsisitiza Rais Samia, kama anaweza kuacha alama ya katiba kabla ya 2025, atakuwa amefanya jambo jema ili hiyo 2025, hata asipo, atakuwa ameacha alana!.

Otherwise lets put our fingers crossed and pray for her ili 2025 awe Samia, Tanzania na Watanzania tumfaidi Rais Samia kikamilifu!

Mungu Mbariki Rais Samia aendelee 2025,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu uwezo wa wanawake kwenye uongozi
 
Wanabodi,
Kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo makala yangu ni makala ya dhana dhanifu, kuhusu Tanzania ya 2025 -2030.

Makala ya leo kwanza inafundisha kujua types tatu za leaders, kuna born leaders, na made leaders, na kwenye made
Andiko zuri Lina kasoro za kutopendwa kuambiwa ukweli Ili hali we ni mwanadamu, kubali usemwe pale unapoonesha uchawa katika Dunia inayoona yakuwa ni aibu Kwa mtu mzima kama wewe kuwa chawa wa dada ambae ameshindwa kuongoza Bunge jinsi tutakavyo watanzania, Kwa KIFUPI Kumsifia mtu anae jisaidia pembeni mwa shimo la choo Ili hali shimo lipo na lipo tayari kupokea uo ni uchawa Tena uchawa wa kijinga,Kuliko kupitisha bajeti mpya Ili majizi yaendeele kuiba,ni vyema wangejadiki majizi Ili yakamatwe tupitishe bajeti iende Kwa walio wasafi!

Andiko lako Lina elimisha ila uliko mweka Madame president siko hata iweje hatoacha kulipa shukurani tambua Kwa Sasa analipa shukurani Kwa walio mweka madarakani yeye na Marehemu Magufuli,(kuwa na adabu Mpe heshima yake ya Sasa anaitwa marehemu Magufuli usimtaje kana kwamba upo nae unakunywa nae kahawa au mbege).

2025-30 hakutokuwa na badiliko lolote lenye tija Kwa WANANCHI lazima wenye nacho wataongezeka kama ilivyo Sasa Kwa kuwa unakuwa chawa Kwa Sasa tegemea teuzi maana nawe SI washiriki kuwafanyia kampeni za kuwarubuni watanzania yakuwa wamchague mambo yatabadilika?

Hacha ngariba za kutudanganya ccm imeisha choka itoke madarakani mwandishi mwenye hekima Kwa Tanzania ya Leo iliyojaa mijizi ndani ya mfumo atatumia kalamu yake vyema kuwambia ukweli watanzania.


Msingi wa nyumba ulio jengwa na Baba Pascally ukaja kumalizia nyumba na Mama Pascally kusimfanye Baba Pascally aonekane hakufanya jema ila jema limefanywa na mama pascally.

Jipi jipya litaje aliro anzisha mama yako?hakukuta elimu Bure?kama UNAAMBIWA hata barabara mpya hata moja hajajajenga ila anaziba viraka hata ilo ulioni?soko gani jipya kajenga?hakukuta COVID 19 wanalipwa SI kaendelea kuwalipa? Hakukutaba Mwendazake amekopa yeye hajakopa? Nitajie jina la mkulima kutoka mwanalumango au itongo au rubya au kisana,himo au marangu aliye alikwa ikulu kula futari Ili nikutajie majina ya vijana tulio soma nao Darasa moja tukaishi nao ostabey wakapata bahati wakaingia kweny e idara nyeti na Sasa ni mapunga huko marekani wanapakuliwaaaaaaaa!
 
Je wajua kuwa licha ya Tanzania na Watanzania kumfaidi Rais Samia kwa makubwa anayoyafanya sasa, anayafanya japo ni born leader lakini ameupata urais kwa manmade na God made leader, hivyo kama sasa tuu hivi alivyo amefanya makubwa na anaendelea kufanya mambo makubwa mazuri ya kupendeza, sii wengi wanajua kuwa tutamfaidi zaidi Rais Samia iwapo ataendelea na urais wa 2025 - 2030, kuliko sasa?.
Bold: Kuna "research gap" hapa. Asante.
 
Wanabodi,
Kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo makala yangu ni makala ya dhana dhanifu, kuhusu Tanzania ya 2025 -2030.

Makala ya leo kwanza inafundisha kujua types tatu za leaders, kuna born leaders, na made leaders, na kwenye made
Machawa mnatuchosha na ngonjera zenu. Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu tangu aingie madarakani. Kila kitu kimepanda bei zaidi ya mara mbili, wizi, ufisadi maradufu. Acheni ujinga wenu bana.
 
Wanabodi,
Kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo makala yangu ni makala ya dhana dhanifu, kuhusu Tanzania ya 2025 -2030.

Makala ya leo kwanza inafundisha kujua types tatu za leaders, kuna born leaders, na made leaders, na kwenye made leaders kuna manmade leaders na Selfmade leaders. Na ndani ya makundi hayo makubwa mawili kuna sub groups za
Umemuweka mkapa kwenye born leaders...unaakisi tatizo lilelile la wasomi wa Tanganyika na vifuniko vya 'imani' kwenye 'macho' yao...bila Nyerere mkapa asingekua rais,kudai hakuwa na 'wa kumlipa fadhila' si kweli,alikalia kitu sababu ya dhehebu lake na alipaswa kulipa fadhila' kwa Nyerere (i.e kanisa lake)...hakumzidi sifa za urais mzee malecele iwe kielimu,uzoefu na hata umashuhuri chamani achilia mbali siasa zenyewe
 
Back
Top Bottom