Wajane wawili wauawa Kyela kwa tuhuma za kusambaza kipindupindu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,367
Wajane wawili wa Kitongoji cha Bulinda wilayani Kyela wameuawa kwa mapanga wakidaiwa kusambaza ugonjwa wa kipindupindu baada ya kufiwa na waume zao katika eneo hilo.

Waliouawa ni Geneli Kapwela (65) na Rahabu Bungulu (70) waliokuwa wakiishi peke yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema jana kuwa wajane hao waliuawa juzi baada ya
kipindupindu kuhusishwa na imani za kishirikina.

Takwimu za mauaji toka polisi zinaonyesha karibu watu wawili wanauawa mkoani Mbeya kwa imani za kishirikina
 
Kha.......kipindupindu nacho imekuwa ushirikina...????
 
Hii stori niya muda mrefu sana zaidi ya wiki mbili nashangaa Jf mmeiweka Instagram kama new stori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…