a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 420
- 730
Familia yako ukiijali na kuipa kipaumbele ni baraka ,na jambo jema.Kuna baadhi ya wazazi hutelekeza familia zao na kutozipatia matunzo na malezi.
Wengine hubagua watoto na kuwatelekeza watoto waliowapata nje ya ndoa. Wengine wenye uwezo huwatelekeza wazazi wao kijijini kwao na hukataa kuwasaidia wazazi shida zao zilizo ndani ya uwezo wao.
Wengine wakishafika mjini hukataa kwao au huwakataa wazazi wao kabisa.
TUNAKUMBUSHWA KUWA.
Wewe unaweza kubadilishwa hapo kazini kwako siku ukidondoka ,ukifukuzwq,ukiugua,au ukifa,ukipata ulemavu na akaajiriwa mtumishi mwingine kwenye nafasi yako ambaye anaweza akawa bora kuliko wewe na ukasahaulika ndani ya siku chache.
Lakini thamani yako kama mzazi kwa watoto wako ,au mtoto kwa wazazi wako ni tofauti na kwa marafiki zako,michepuko au kazini kwako.
Wakati wa shida ni rahisi familia yako ikasimama na wewe mwanzo mwisho kwenye dhiki,maradhi kuliko kwa watu baki wengine nje ya familia yako.
Ni vizuri kuwekeza muda ,upendo,kuwatunza kuwajali na kuwathamini na kuwalea wa nyumbani kwako,kuliko marafiki au michepuko au kazini/kazi.Kutumia au kufuja fedha na muda mwingi kwenye anasa na starehe za dunia na kuwatelekeza wa nyumbani kwako.
Pia wadada wa kazi (HAUSI GELI /beki tatu)wanotuangalizia nyumba na watoto tukiwa makazini. Ni vizuri kuwajali na kuwathamini kama sehemu ya familia na si kama mtu baki.