Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,355
- 56,755
Ni dhahiri bila chembe ya shaka, Waislamu walikuwa msitari wa mbele kumng'oa mkoloni. Hilo halina ubishi, maana Tangu enzi za vita vya mababu zetu dhidi ya wakoloni, struggle nyingi zilifanyika kwenye ukanda wenye waislamu wengi, kuanzia kwa Mkwawa, Abushiri huko Pangani, Kinjekitile Ngwale huko Kilwa wote hao walikuwa Waislamu (Anayetaka elimu ataelimishwa).
Harakati za Uhuru nazo kwa kiwango kikubwa zilikomaa zaidi katika mikoa ya waislamu wengi, kuanzia kwa vyama vya AA, kuja TAA hadi TANU, Majority ya waliounga mkono struggle hizo walikuwa ni Waislamu.
Baada ya Uhuru Nyerere aligundua kuwa nguvu mojawapo inayoweza kumsumbua kutawala ni Waislamu, kwa hiyo akawatengenezea chombo chini ya Usalama wa Taifa kiitwacho BAKWATA, chombo hiki kazi yake ni kuhubiri amani, na kukataza movement yoyote ya waislamu kuraise up.
Kitu kimoja ambacho Nyerere alisahau au aliacha kwa makusudi ni kuliacha Kanisa kuoperate nchini kwa Autonomy, bila kuingiliwa organisations zake na mipango yake. Kitabu cha Sivalon cha Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania kilitoa mwanga namna ambavyo kanisa lilikuwa likishirikiana na serikali. Nyerere mwenyewe amewahi kutamka kuwa "I have given the church, a good chance to operate in Tanzania". Matokeo ya sera za Nyerere za kuwacontrol waislamu kupitia BAKWATA na Kuliacha Kanisa Kuthrive, leo hii limetengeneza Power Kubwa sana ya kimtandao na waumini wengi kiasi kwamba Likiamua jambo dhidi ya serikali kwa dhati ya kuliamua basi serikali ya bongo haina namna zaidi ya kukaa chini kuzungumza nalo ama kwa siri au kwa dhahiri (Huwa kuna mikutano mingi tu serikali huwa inafanya na maaskofu kimyakimya).
Sasa Kanisa linataka haki nchini, limechoshwa na propaganda za Amani. Linataka amani ya kweli itamalaki kupitia Haki. Polepole limeanza kupaza sauti. Kwa bahati mbaya Kanisa si BAKWATA, Kanisa si tawi la Serikali, Halitabiriki, linaweza kuiunga mkono serikali waziwazi au likaamua kuigomea, na serikali haina uwezo kulifanya lolote!.
Na bahati nzuri kanisa limejijengea heshima kwa:
1. Kumchenjia Magufuli alivyokuwa anakandamiza demokrasia, kumbuka ule waraka wa demokrasia uliomchanganya Magufuli, hivyo hii inaondoa dhana kuwa Kanisa linabaugua mtawala wa kumkosoa kwa misingi ya dini yake.
2. Waraka wa Covid, uliotaka serikali iache kufanya mambo kama waganga wa kienyeki huku wananchi wakiwa hatarini
3. Hata maaskofu kama Niwemugizi, Bagonza, Saba na wengineo walisimama kiume na kutoa kauli kuwa mambo hayako sawa
Alivyokuja huyu mama na kuanza kuingia mikataba ya kimangungo kwa kuuza bandari yetu kanisa lilisimama na kukataa. Hata hivyo halikuamua kuwapeleka mamilioni barabarani kwenda Ikulu ili "kuleta misa" ya kuombea busara kwenye matumizibya rasilimali zetu. Uwezo huo linao lakini halijaamua tu.
Sasa, kwa sasa Baada ya Serikali kufanikiwa kuwazima Waislamu kupitia sheria za Ugaidi, Kuwatia ndani na kuwashughulikia Masheikh influential, Kuvamia misikiti na kusimika maimamu wanaowataka kupitia operation maalum za usalama wa Taifa, Na kuwaweka kwenye payrol baadhi ya masheikh, Serikali imefanikiwa kudhibiti mwamko na nguvu za Waislamu. Waislamu wa leo siyo sawa na Waislamu wa Mwembechai mwaka 1998, Wale walikuwa breed nyingine kabisa. Wa sasa wamethibitiwa!.
Ila Kanisa lipo Strong, Kama kuna Taasisi itakayoharakisha CCM kudondoka ni taasisi ya Kanisa (TEC). Ugumu wa kudeal na Kanisa ni kuwa kuna waumini wao wengi ktk mifumo ya nchi na serikali, ni vigumu nyakati zote kuwa loyal kwa mifumo kandamizi ya kiutawala huku wakiendelea kuwa members wa taasisi za dini zinazowanyooshea vidole, lazima crack ktk dhamiri zao itakuwepo. Uwezo wa kiorganizesheni wa Kanisa kufikia mtu wa chini, Loyalty ya waumini kwa viongozi wa dini, Lakini kikubwa zaidi ni Waumini, hawa ni nguvu ambayo Kanisa ikisema iitumie kukataa mambo ya kiuonevu ya CCM, basi CCM haina chance.
Ukombozi wa Kwanza wa nchi hii kwa kiasi kikubwa uliungwa mkono na umma wa waislamu kwanza na zaidi, Ila ninaona ukombozi wa pili wa nchi hii utaletwa na Kanisa!