Naomba kuuliza CCM kama chama tawala na kilichoshika hatamu, kina mpango mkakati UPI Juu ya wale wanaojitokeza kuwania uenyekiti Wa jumuiya ya vijana na nafasi nyingine?
Maana uvccm ni tanuru la moto la kupigka viongozi Wa chama na Serikali.
Je haioni umuhimu Wa kuanza kuwafuatilia vijana waliojitokeza mwaka 2008 kuwania uongozi Wa jumuiya hiyo na kuwatumia sasa katika nafasi mbali mbali? Maana wengine wametelekezwa tuu na chama hakijui walipo.
Maana 2008! Na nani vijana wengi wenye Akili timamu na uwezo Wa kuongoza walijitokeza kama vile Pangisa haule, said sambala, said mtanda na Esther bulaya, hakuna kosa kubwa kama kuwasahau na kutowathamini maana wakijiunga vyama binzani wanakuwa Msiba kwa Serikali na chama,
Rai yangu kwa Serikali naomba tuwe tunapitia data base na kuwaangalia wapo wapi na wanafanya mini?
Mfano haule Pangisa alifanya kazi nzuri sana alipokuwa chuo cha uhasibu Arusha na alinihamasisha Mimi kujiunga na CCM na alipomaliza chuo chadema wakaingia na kuizidi nguvu CCM.
Chama na Serikali tuamke na kuwatumia hao vijana wetu kadri ya uwezo wako na taaluma zao.
Pepo ya mabwege .com