Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wawili wa ACT-Wazalendo wawajia juu Maalim Seif na Zitto Kabwe kwa kumuunga mkono Tundu Lissu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,201
5,585
WAGOMBEA wawili wa kiti cha Ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo kupitia majimbo ya Kibamba jijini Dar es Salaam na Kyerwa mkoani Kagera wamewajia juu viongozi wa chama hicho kutokana na kauli yao ya kumuunga mkono mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu.

Wakizungumza katika mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Wagombea hao Mwesigwa Siraji wa Kibamba na Ntareyeiguru Frederick wa Jimbo la Kyerwa, kwa pamoja walisema kauli ya viongozi wao hao hazikubaliki na kwamba zimekiuka misingi ya katiba ya chama hicho.

Alisema wakiwa kama wagombea na wanachama wa chama hicho, hawawezi kulazimishwa ghafla 'kumpigia' debe Lissu hali yakuwa chama hicho kinaye mgombea wake wa nafasi hiyo ya Urais Bernard Membe ambaye kwa mujibu wao anakubalika maeneo mengi nchini.

"Kwa utafiti tulioufanya Membe atapata ushindi mkubwa kutokana na kukubalika na wananchi wengi, cha kushangaza wao wanamuacha na kushinikiza watu tumuunge mkono Lissu" alisema Siraji

Alisema kwa mujibu wa kifungu kilichopo ukurasa wa 21 wa katiba ya ACT Wazalendo, ni kinyume na utaratibu kwa mwanachama yoyote kumuunga mkono au kumpigia debe mtu kutoka chama kingine ambapo kwa kufanya hivyo mtu huyo anakuwa amejifuta uanachama ndani ya chama hicho.

Alisema kwa misingi hiyo, Kiongozi Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe pamoja na Mwenyekiti wao Maalim Seif Sharif Hamad wanakosa sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo kwa kitendo chao cha kumnadi mgombea wa Urais wa CHADEMA Tundu Lissu.

"Kutokana na hatua hiyo tumepanga jumatatu tutakwenda kufungua kesi mahakamani kule Zanzibar ili ichukue hatua ya kumvua Maalim Seif nafasi yake ya kugombea Urais kutokana na kukosa sifa" aliongeza Siraji

Kwa upande wake Frederick alisema wao kama wanachama wa chama hicho wanalaani kitendo cha viongozi hao kuamua kumkacha mgombea wao Membe hali ya kuwa walimpitisha wao kuwania urais kupiti chama hicho.

"Isitoshe Membe alishiriki kwa ziadi ya asilimia 75 kuandaa ilani ya chama ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu, leo wanajitokeza hadharani kusema hawamtambui, hiyo siyo kweli sisi bado tupo naye hadi mwisho wa uchaguzi" alisema Frederick

Alisema wao kama wabunge wanaendelea kumuombea kura Membe katika majukwaa yote wanayosimama na imani yao ni kwamba atashinda kiti hicho licha ya hujuma anazofanyiwa na viongozi hao wa juu wa chama hicho.

Aidha kwa pamoja walikionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kisitarajie mteremko katika nafasi zote kwa kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinaibuka na ushindi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

1603463663732.png


Pichani kulia ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibamba kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo,Mwesigwa Siraji akionesha kitabu cha Katiba yao ya chama hicho mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambayo amedai kuwa viongozi wake wa juu wanaikiuka na wao hawatokubali.Mwesigwa amesema kuwa wakiwa kama wagombea na Wanachama wa chama hicho, hawawezi kulazimishwa ghafla kumpigia debe Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu hali ya kuwa chama chao kina Mgombea Urais Ndugu Bernad Membe anaetambulika kisheria.Kushoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyerwa,Ntareyeiguru Frederic.

Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyerwa, Ntareyeiguru Frederic akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),kuhusu kulaani kitendo cha viongozi wa chama hicho kuamua kumkacha mgombea wao Mhe,Membe hali ya kuwa walimpitisha wao kuwania urais kupiti chama hicho."Isitoshe Membe alishiriki kwa ziadi ya asilimia 75 kuandaa ilani ya chama ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu, leo wanajitokeza hadharani kusema hawamtambui, hiyo siyo kweli sisi bado tupo naye hadi mwisho wa uchaguzi" alisema Frederick
 
Ndo dk 89 za Membe hizi sio?
ACT ilikosea sana kumkaribisha Membe
Sasa mtu haonekani week tatu tangu kampeni zianze ulitegemea viongozi wafanye nini zaidi ya kuumga mkono Tundu Lissu
 
Basi waendelee kumpigia debe mzee wa goli la dakika ya 89
Hao jamaa wanaopiga kelele kwamba Membe amesalitiwa watashangaa pale ambapo Membe atawashangaa kwa kubishana na viongozi wa juu
Ninatabiri kwamba Membe hatimaye atakubaliana na Zito na Maalim hapo ndio utajua siasa haitaki msimamo mkali
 
Dah! Sijui wamevuta bei gani kutoka kwa sloslow. Mzahazaha hivi hivi watu wanatolewa kwenye reli.
Hamna kesi hapo mlengwa ni Maalimu, wakienda kufungua kesi Zanzibar itakuwa batili kwakuwa wao siwapiga kura wa Zanzibar.
Pili hiyo kesi ikianza j3 itaisha ijumaa ambapo tayar Maalimu atakuwa raisi

Tatu :Hakuna sehem Maalimu au zitto waliwahi kusema kuwa wanamuunga mkono Lissu ila zitto yeye binafsi atampigia kura Lissu na maalimu anaimani kuwa Lissu anashinda
 
Nilimsikia Seif Sharif kuwa maamuzi ya kumuunga mkono Lisu yalifanywa na kamati Membe akiwemo.

Zitto na Maalim sio wao peke yao wafukuzwe kuwa wanachama wa ACT-WAZALENDO na MEMBE pia.

Pengine na waliohudhuria kwenye hicho kikao cha kamati wafukuzwe,hao waliounda hiyo katiba Wafukuzwe.

Kwa ufupi katiba imeundwa na kamati,kamati hiyohiyo imeamua kupindisha baadhi ya vipengele.

Kumbuka Katiba sio MSAHAFU.

Mwaka huu CCM,kimewaganda.
 
Hamna kesi hapo mlengwa ni Maalimu, wakienda kufungua kesi Zanzibar itakuwa batili kwakuwa wao siwapiga kura wa Zanzibar.
Pili hiyo kesi ikianza j3 itaisha ijumaa ambapo tayar Maalimu atakuwa raisi

Tatu :Hakuna sehem Maalimu au zitto waliwahi kusema kuwa wanamuunga mkono Lissu ila zitto yeye binafsi atampigia kura Lissu na maalimu anaimani kuwa Lissu anashinda
Kwiiiiiiiii kwiiiiiiiiiii. Njia ya mwongo fupi wakati lisu anamnadi mgombea wa ACT alipokuja aapa zenji, malimu seifu naye halikadhalika akajaaa ndani ya 18 kwa kumnadi lisu. Halafu ZITO ZUBERI KABWE LUYAGWA akasema atampigia lisu kula yake, kwani walikuwa hawajui kama nikinyume na katiba ya ACT? Tulieni sheria ishike mkondo wakee.
 
Yale Yale ya Pro, LIPUMBA na Dokta Slaa, ya kununuliwa na MaCCM ili KUVURUGA na KUUA UPINZANI,
Yalianzaga hivi hivi kama mzaha vile.
Membe Mungu anakuona.
Huyu Lissu mwenyewe aliwahi kutamka kuwa ACT sio chama cha upinzani ni kwamba kimeundwa ili kuvuruga upinzani,sasa nikashangaa Lissu tena aliyetamka maneno hayo anashirikiana na ACT.

 
Sawa kabisaa. Tena wakatafute haki zao kwenye vyombo husika maana wametapeliwa kisiasa

Vile vyama vya upinzani hawana dira wanataka kuvuruga hadi wanachama wao wenye malengo sababu ya uchu wao
 
Back
Top Bottom