Wagombea Mbowe anayetetea nafasi yake, Lissu na Odero kufanyiwa usaili leo ofisi za Chadema

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,945
5,289
Wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Chadema, wanafanyiwa usaili leo Jumapili, Januari 19, 2025, ikiwa ni maandalizi ya kinyang'anyiro cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumanne Januari 21, 2025.
IMG_2598.jpeg

Usaili wa wagombea hao, unafanyika yalipo Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni jijini Dar es Salaam na tayari wagombea mbalimbali wameanza kuwasili.

Wagombea wanaofanyiwa usaili huo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar na Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Wanaogombea nafasi ya uenyekiti ni Freeman Mbowe anayetetea nafasi hiyo, Tundu Lissu na Charles Odero.

Hadi saa 4:30 asubuhi, Odero ndiye mgombea uenyekiti pekee aliyekuwa amefika katika ofisi hizo, akisubiri taratibu za usaili, huku Lissu na Mbowe bado hawakuwa wamefika

Soma, Pia:

- Mwanaharakati Odero Charles Odero ajitosa kuwania nafasi ya Uenyekiti CHADEMA Taifa
 
Back
Top Bottom