Danielmwasi
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 2,098
- 3,721
Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imewakabidhi Raia wanne wa kigeni vibali na kadi za utambulisho wa kuishi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla baada ya baadhi ya kanuni za uhamiaji kuruhusu Wageni walionunua nyumba Zanzibar zenye thamani ya dola laki moja za Kimarekani ( zaidi ya milioni 250 ) wapewe vitambulisho hivyo vya Makaazi.
Serikali ya Zanzibar ilipendekeza sharti hilo kama kivutio kwa Wageni kununua nyumba Zanzibar ambapo yeyote atayenunua nyumba kwa dola laki moja za Kimarekani ataruhusiwa kukata kibali cha kupata kitambulisho kitakachomtambua kuwa ni Mkaazi wa Zanzibar.
@AyoTV_ imefahamishwa kuwa kitambulisho hicho ambacho kitakua cha matumizi ya muda wa miaka miwili kitatolewa kwa dola 550 (Tsh. milioni 1.4) kwa Wageni kutoka Nchi nyingine huku Wageni kutoka Nchi za Afrika Mashariki wakilipia dola 300 za Kimarekani ( Tsh. 776,851).
Masharti mengine yaliowekwa na Mamlaka ya ZIPA na Uhamiaji ili Mgeni kuupata kitambulisho huo ni uthibitisho wa nyumba iliyonunuliwa kwa dola laki moja, TIN namba ya Mnunuaji wa nyumba hiyo, uthibitisho wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar ZIPA pamoja na uthibitisho kutoka Polisi.
Wageni hawa wanne waliopewa vibali hivyo leo wote ni Raia wa Uholanzi ambapo hii inakua ni mara ya kwanza kutolewa kwa vibali hivyo vya ukaazi Visiwani Zanzibar na vitaendelea kutolewa kwa Wageni wataokidhi vigezo vilivyowekwa. #MillardAyoUPDATES