Wageni Hawaendi Ugenini Kwenda Kuwajenga Wenyeji

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,102
45,528
Ni ukweli wa kimantiki, wageni wahamiaji wanaenda mataifa ya ugenini kwenda kutafuta maisha, siyo kwaajili ya kwenda kuyajenga mataifa hayo waliohania wala kuwaebdeleza wananchi wenyeji.

Ndiyo maana mataifa mbalimbali huweka sheria kwaajili ya wageni Na wageni hawa wawapo katika mataifa ya ugenini, hunyimwa baadhi ya haki ili kuwazuia wageni hawa wasio na uchungu kwa wenyeji na Taifa lao, wasifanye uovu wa kuwanufaisha wao binafsi, kwa gharama ya wenye Taifa lao.

Mataifa yote Duniani, yanawazuia wageni kuomba uongozi, kupiga kura, kuomba kuchaguliwa au kuweza kuteuliwa kuongoza taasisi za umma.

Tatizo kwa Taifa letu, limekuwa ni kama Taifa lisilo na mwenyewe. Wageni wanaingia bila hata ya kufahamika. Wakiwa bado ni, wakishachuma mali, wakapata hela ya kuwahonga wajumbe wa CCM kwenye kura, tayari wanakuwa viongozi wa CCM, wabunge na wakiuoata ubunge wanakuwa mpaka mawaziri. Wakiwa mawaziri, wanatumia nafasi hizo za uwaziri, kuwanufaisha wahamiaji haramu wenzao. Yaani sasa wahamiaji haramu wanakuwa na haki zaidi ya rasilimali za nchi kuliko wenye nchi.

Sasa tuna viongozi moaka ngazi za juu kabisa Serikalini, ambao kwa mujibu wa sheria, ni wahamiaji haramu. Hawa wahamiani haramu, kwa mujibu wa sheria, hawakustahili kuchagua, kuchaguliwa wala kuteuliwa, kwa sababu tangu wazazi wao waingie nchini, si wazazi wao wala wao wenyewe waliowahi kuomba uraia na kupewa, kama sheria zinavyoelekeza.

Tufahamu kuwa watu hawa ambao kisheria siyo raia wa Tanzania, lakini wameweza kuchukua uongozi katika nchi hii, kamwe hawataliacha lengo kuu la wazazi wao wao na familia zao, ambalo lilikuwa ni kuchuma mali.

Kadiri hawa wahamiaji haramu wanavyozidi kuongezeka kwenye nafasi za uongozi, lazima tufahamu kuwa ufisadi, uporaji wa rasilimali asilia za nchi, na wizi ndani ya Serikali utazidi kuongezeka. Lakini kwa upande mwingine, kama alivyotahadharisha mkuu wa majeshi, kiusalama nchi yetu inazidi kuwa hatarini.

Kwa sababu Serikali ya CCM imeamua kuuweka usalama wa taifa mashakani, kuanzia kwenye Serikali za mitaa, mpaka uchaguzi mkuu, wananchi wasithubutu kumpa uongozi mtu ambaye kisheria siyo Mtanzania. Na hawa watu wakidiriki kupora mamlaka ya umma katika kuwachagua viongozi wanaowataka, wananchi wachukue hatua mikononi mwao dhidi ya huyo waliyeletewa bila ya kumchagua wao. Ni aheri nusu shari kuliko shari kamili.

Na kwa mawaziri, wabunge na baadhi ya viongozi wa CCM, ambao mnajifahamu kabisa kuwa ninyi kisheria siyo raia, kama mna nia ya kuwa Watanzania, fuateni taratibu za kuupata uraia, mkipuuza, kuna siku mtajuta.
 
Back
Top Bottom