Wafuatao wajiandae kumrithi Rais Dkt. Magufuli mwaka 2025 tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Wakijilinda Kiafya na kuzidisha sana maombi yao ya Utendaji huku wakiwa waaminifu na wenye moyo hasa wa Kiuzalendo na Mapenzi ya dhati kabisa kwa nchi ya Tanzania basi wafuatao watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Dkt. Hussein Mwinyi
Makamu wa Rais Jennister Mhagama
Waziri Mkuu Suleiman Jaffo

Endapo hao Watajwa hapo juu Mwenyezi Mungu hatotubariki kuwa nao hadi huo mwaka wa 2025 basi wafuatao wajiandae kuchukua nafasi zao endapo tu na Wao watalinda afya zao, kuzidisha maombi yao kwa Mwenyezi Mungu, wakiwa waaminifu hasa bila kusahau wawe Wazalendo wa kweli kwa nchi ya Tanzania basi watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Professor Makame Mbarawa
Makamu wa Rais Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu Luhanga Mpina

Ombi kwa Watajwa hao hapo juu tafadhalini......
  • Tunzeni afya zenu ( HILI NAOMBA MLIZANGITIE SANA )
  • Jiheshimuni sana ( maisha ya Kihuni / Kisela / Kisanii sasa kaeni nayo mbali )
  • Zidisheni uadilifu wenu
Ombi langu Kuntu kabisa kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli juu ya hawa Watajwa ni kwamba.....
  • Waamini sana hao niliowataja hapo juu
  • Wazidishie Ulinzi wao kwani ndiyo Warithi wako wazuri na watarajiwa
  • Wajenge zaidi hasa Kiitifaki
Kila la kheri na ni matumaini yangu makubwa Kwako Mheshimiwa Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Magufuli kuwa Mimi GENTAMYCINE nimekurahishia Kazi yako ya kuwakabidhi nchi akina nani hapo mwaka 2025 utakapong'atuka na hao ndiyo pekee watakaokufaa kwani wana uthubutu wa kupita mule mule ambako umepita Wewe na kuzidi kuiletea Maendeleo hii nchi yetu.

Nawasilisha.
 
Mkuu Ummy Mwalimu ni MTanga siyo Mzanzibar, katiba inasema makamu wa rais shart atoke Zanzibar
 
GENTAMYCINE mara hii umegeuka mpiga ramli chonganishi!!!! Haujui kuwa unachonganisha na wenzao.

2020 Mwinyi ndio Rais wa Zanzibarrrrrrrrrrrrrrr . . .....................Over
 
Makonda hayupo? Lizaboni, Barbarossa, Wakudadavua, Troll jf

Nimeweka Kitu cha Kiutafiti, Kiuchambuzi na cha Kimkakati hasa wa Ushindi kwa CCM huo mwaka 2025. Hao wakiteuliwa na Chama kama nilivyoainisha hapo halafu wakajipanga kama nilivyopanga basi Tanzania itaendelea kufurahia Uongozi mzuri wa Chama Tawala (Chama changu pia) cha CCM kwani nawaamini 100% hao Watajwa na nawakubali mno. Ukiona hadi GENTAMYCINE anakukubali jua hata Mwenyezi Mungu ameshakuwekea tiki na amekukubali kwani Mimi ni Malaika wake wa Kutukuka kabisa hapa duniani.
 
Hivi .....kwani 2020 hakuna uchaguzi!? Experience ni muhimu lakini sio kwa kujiondoa ufahamu kiasi hiki.
 
Makonda hayupo???Lizaboni,Barbarossa,Wakudadavua,Troll jf

Nimeweka Kitu cha Kiutafiti, Kiuchambuzi na cha Kimkakati hasa wa Ushindi kwa CCM huo mwaka 2025. Hao wakiteuliwa na Chama kama nilivyoainisha hapo halafu wakajipanga kama nilivyopanga basi Tanzania itaendelea kufurahia Uongozi mzuri wa Chama Tawala ( Chama changu pia ) cha CCM kwani nawaamini 100% hao Watajwa na nawakubali mno. Ukiona hadi GENTAMYCINE anakukubali jua hata Mwenyezi Mungu ameshakuwekea tiki na amekukubali kwani Mimi ni Malaika wake wa Kutukuka kabisa hapa duniani.
 
Watanzania kwa asilimia 100% hakuna aliye mtabiri JPM kukamata madaraka haya makubwa aliyo nayo.

Wengi tulimfikiria Lowassa na baadae B. Membe.

Hivyo kama ni Utabiri, ama ni ndoto umelala ukaota hivyo, ni bora mleta mada ukaendelea kulala tu, ili kuimarisha na pengine kufanya ndoto yako kuwa ya kweli.

Kila la kheri kwa wote ulio wataja kuongoza/kutuongoza kesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo tunasema other factors remain constant. kitokea maono ya LEMA yakitimia basi SAMIA mpaka malengo ya millennium yatimie 2025 plus 10 years, ila sijui hesabu nilikuwa napenda sana hisabati, then kuna tofauti ya kuota na maono ila zote ni ndoto na silazima zitokee ila zitasemwa na kuendelea kutamkwa pia uchochezi sio lazima uende kisongo ata keko wachochezi wapo, huru wa habari ni tofauti na uhuru wa kuongea unaruhusiwa na katiba wasioitaka ukawa (nawaza tu kama mjinga msinihukumu)
ngoja niendelee kuota ndoto zitimie
 
Back
Top Bottom