Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,092
- 728
WAFANYAKAZI WA UBALOZI WATEMBELEA MJI MKONGWE WA COMORO
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro wametembelea mji mkongwe wa Comoro na kujionea maeneo yanayoweza kuwa na ushirikiano na Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Wafanyakazi hao wakiongozwa na Mhe. Balozi Saidi Yakubu pia wamejionea Tamasha la picha mbali mbali zilizokuwa kivutio kwa wageni mbali mbali waliohudhuria akiwemo Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja, Ibrahim Mze.
Katika ziara hiyo, waliweza pia kutembelea makazi ya aliyekuwa Mtawala wa Visiwa hivyo, Sultan Bin Ahmed Mwinyi Mkuu na baada ya kukamilika kwa ziara, Mhe. Balozi Yakubu aliwaahidi waratibu na wenyeji kuwa maombi yao ya ushirikiano na Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar yatafikishwa kwa hatua zaidi.
Eneo la Bajanani ulipo mji mkongwe wa Comoro lina historia ndefu ikiwemo kuwa ndio la mkusanyiko wakati wa harakati za uhuru wa Comoro.