Wafanyakazi wa TIGO-Tanzania wanashiriki kutapeli pesa wateja wao?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
28,410
39,486
Habarini Wadau,

Najua wazi hili linaweza kupingwa na wengi especially Staffs wa kampuni ya Mtandao wa simu ya TIGO, Lakini nakusudia kuweka wazi situation ya UTAPELI kwa njia ya Mtandao unaofanywa na baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni hii.

Kabla sijaeleza vizuri hali iliyotokea kwa mwaka Jana na Mwaka huu hasa Mkoani Kilimanjaro, jaribu kusoma malalamiko ya Wateja wa TIGO kuhusu UTAPELI kuanzia mwaka 2010 mpaka 2021.

Hata hapa wapo Wadau walioandika kuwa wanakwenda kuishtaki kampuni ya TIGO kwa UTAPELI huu.

UTAPELI huu sio wa vifurushi isipokuwa ni wa KUHAMISHA PESA kutoka kwenye Account za wateja na kwenda kwenye namba wanazozisajili na kisha kufutia USAJILI mara baada ya kufanya Utapeli wa kuhamisha pesa.

SWALI: KUNA USHAHIDI GANI KUWA NI WAFANYAKAZI WA TIGO.

Ushahidi upo wazi kwasababu kuna UTAPELI umefanyika Kilimanjaro na mmoja kati ya waliofanya utapeli alikuwa na kitambulisho active cha kazi pamoja na Uniform za Tigo na pia amehusika katika Kusajili Line, kufanya Transaction ya Pesa na baadae kufuta USAJILI wa line hiyo.

UTAPELI huu umeripotiwa Polisi katika mamlaka husika lakini kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Baadhi ya Polisi hao nao wanahusika kufanya utapeli na Wafanyakazi hawa, yaani wana Deal moja.

Kwasasa utapeli mkubwa wanafanya kwa Wageni / watalii.

Tunawaomba TCRA mshughulikie suala hili pamoja na Ushirikiano kutoka Polisi kitengo cha Cyber Crime na kampuni ya TIGO pia.

Wadau kuweni makini sana na hivi vibanda vya Tigo na hats Ofisi zao rasmi kwani sio wote wenye nia njema ya kuwasaidia.
 
Ambatanisha na ushahidi.
Mimi ni mteja wa mtandao pendwa na sijawahi kupigwa zaidi ya kuenjoi ma gb ya kufa mtu..

Screenshot_20220225-092843.png
 
Hao ni mawakala/freelancer.uo utapeli upo mitandao yote.
Kuna namna nyie wenyewe mnawatajia namba za siri bila kujua.
 
Haingii akilin hata kidogo usajili kwa kidole chako halafu aliyekusajilia afute hicho kitu unachozumza sio kweli inatia shaka kido ifutwe line iliyosajiliwa kwa alama kidole chako ulisema ulinunua line iliyosajiliwa tutakuelewa na kwanini ununue isiyokuwa na taarifa zako mtoa mada unanipa mashaka kidogo kwenye maelekezo yako
 
Na utapeli mwingine ni kuwa mwezi Julai mwaka jana ktk maonyesho ya 77 TIGO waliniuzia simu na kunihaidi kuwa kila mwezi watakuwa wananipa GB 2 za bure. Lakini tangu mwezi uliofuata sijawahi kupata offer hii licha ya kufuata masharti yao na kufuatilia ktk ofisi zao na za wakala mara kwa mara. Sasa siwaamini tena na promo zao. Wafanyakazi walioshughulikia jambo hili nina majina yao na vituo vyao.
 
Pole Sana mkuu
Ila hao wafanya kazi wao ndiyo wezi me nakumbuka Kuna jamaa ambaye alikuwa mfanya kazi wa tigo, aliniambia kupitia hizo simu za promotion huwa wanawapiga Sana wanaozinunua, yaani unakuta zile offa za mb hawampi zote hivyo zilizobaki wanauza kwa watu wengine
Yaani upigaji upo Kila Kona
Upigaji ndiyo ahueni ya mhudumu
 
Haingii akilin hata kidogo usajili kwa kidole chako halafu aliyekusajilia afute hicho kitu unachozumza sio kweli inatia shaka kido ifutwe line iliyosajiliwa kwa alama kidole chako ulisema ulinunua line iliyosajiliwa tutakuelewa na kwanini ununue isiyokuwa na taarifa zako mtoa mada unanipa mashaka kidogo kwenye maelekezo yako
Mkuu sijui kama umenielewa wewe, hao watu hawaji kwa nia ya kukusajili kwa njia ya alama za vidole, kwa mfano anakuambia anabadilisha line ziwe za 4G na anakuonesha kitambulisho rasmi na amevaa official sare ya kampuni ya Tigo
 
Mkuu niamini, hakuna mahala ambapo namba ya siri imetolewa
Una uhakika!?
We ni muhanga mwenyewe au unawasemea wahanga!?

Hao matapeli wanaijua kazi yao.
Maana anaweza kusajilia line ya tigo mpya ukaiweka kwenye simu yenye mtandao mwingine labda vodacom,

afu akasema anakuwezeshea huduma ya tigo pesa,Akabinyabinya simu akasema weka namba ya siri,ukaweka namba ya siri ya siku zote uliyoizoea(wengi tunatumia namba ya siri moja sehemu nyingi)

Sasa hapo tayari unakuwa umetoa namba ya siri bila kujua,wewe unakuwa unadhani unaset namba ya siri kwenye line mpya kumbe kakuchomesha unafanya muamala kwenye mpesa.

We mwenyeye shahidi inawezekana una namba ya siri moja mitandao yote!
 
Mkuu sijui kama umenielewa wewe, hao watu hawaji kwa nia ya kukusajili kwa njia ya alama za vidole, kwa mfano anakuambia anabadilisha line ziwe za 4G na anakuonesha kitambulisho rasmi na amevaa official sare ya kampuni ya Tigo
kitambulisho rasmi na amevaa official sare ya kampuni ya Tigo...
😂😂mbona hizo ID na sare yoyote anaweza chonga.
Yani ukiona umetapeliwa ujue wewe mwenyewa umeshiriki kwa 99.999% ila tu hujajua.
 
Back
Top Bottom