Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Zimbabwe wanaendelea na mgomo wao wa siku tatu, kulalamikia kutolipwa mishahara yao. Waalimu, madaktari na wafanyakazi wengine wa serikali wanasema hawakulipwa chochote mwezi Juni.
Uchumi wa nchi hiyo unakabiliwa na uhaba mkubwa wa pesa taslimu kutokana na ukosefu wa mapato kutoka nje, hali ambayo imezidisha hasira miongoni mwa wananchi.
Watu 94 walikamatwa Jumatatu wiki hii, na polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na maji yenye msukumo mkubwa, kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.
Chanzo: DW