MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,064
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.
Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam Buyuni (491), Morogoro Lukobe (25), Shinyanga Ibadakuli (50), Tabora Usule (25) na Mkoa wa Mtwara Mangamba (50).
Aidha kwa Muji wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.
Gharama ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo la Thamani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.
Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu akiwa eneo la jikoni katika moja ya nyumba hizo.
Vigezo vya kununua nyumba hizi ni lazima uwe mwanachama ambaye umechangia makato kwa miaka mitano na zaidi na awe amesajiliwa na mfuko, Lakini pia nyumba hizi zinauzwa kwa fedha taslimu au kwa kutumia nusu ya mafao ya mwanachama kwa wale walio bakisha miaka 5 kustaafu.
Faida kubwa ambayo Mkurugenzi wa PSPF amesema mnunuzi wa nyumba hizi ataipata ni kuwa Nyumba atakayo nunua imekamilika na imejengwa katika uwanja wa ukubwa wa Sqm 800-2500, nyumba ipo katika eneo rasmi lililopimwa na unaweza kupata mkopo wa Benki kwa riba ya asilimia 12.