Dodoma kumejaa,viwanja vya bunge vimefurika.Asasi mbalimbali za kiraia zimefika kutoa maoni yao juu ya miswaada ya dharula iliyoletwa mbele ya kikao cha bunge.TLS ya kina Tundu Lissu haijabaki nyuma,imetuma vijana machachali waliojipa muda kuchambua miswaada hii kwa uweledi mkubwa na kuibua mambo mengi sana ambayo "raia wa kawaida" anaweza asiyaelewe sababu ya kukosa uelewa wa sheria.
Licha ya uzuri wa sababu ya kuleta harakaharaka kwa miswaada hiyo,lakini bado vijana wa TLS wametueeleza kuwa moja ya mapungufu ya miswaada hii,ni kuwa serikali imeweka sheria kuwa mikataba yote ya madini itatakiwa kuletwa bungeni na kujadiliwa,lakini kuletwa kwake bungeni si kabla ya kusainiwa na serikali na wawekezaji,bali baada ya kuwa umeshasainiwa na wadau hao wawili.
Swali linakuja,kuna umuhimu gani au ulazima gani kwa mikataba ya madini,kupelekwa bungeni wakati ikiwa imekwashasainiwa?Kupeleka mkataba uliokwishasiniwa bungeni ili wabunge waujadili,inabadili nini kwa maendeleo ya nchi na mustakhabali wa faida ya rasimali ya madini kwa Taifa?
Hali hii imezua mjadala mkubwa sana,kiasi kwamba watu wengi wamezidi kusema hakukuwa na ulazima kutoa siku chache za kujadili na kutoa maependekezo.Lakini hili la kupeleka mikataba bungeni baada ya kuwa imesainiwa,lina faida gani hasa katika kipindi hiki tunacholalamika kuwa mikataba mingi tumeibiwa??
Sio kila pendekezo litakubaliwaKwani lengo la wao kwenda si ni pamoja na kutoa maoni kuwa IJADILIWE KABLA YA KUSAINIWA? au wamesema maoni ya aina hiyo hayaruhusiwi?
Je watasikilizwa? Kwani umesahau juzi tu nikiwa na maana juzi kweli, wabunge wa upinzani wamesema kuwepo muda wa kusoma na kuelewa kabla ya kutoa maoni, kwani wamesikilizwa. Sasa utapata majibu hata kwa hiyo hoja ndo utaijua vizuri CCM. Watu mkiambiwa mnakuwa wagumu kuelewa, uje unipinge kama hilo halitapakwa mafuta lionekane zuri hata kama wewe umeliona si zuri.Kwani lengo la wao kwenda si ni pamoja na kutoa maoni kuwa IJADILIWE KABLA YA KUSAINIWA? au wamesema maoni ya aina hiyo hayaruhusiwi?
PanyaHii nchi sijui wanaishi binadamu au....?
Najua unaumia sanaHii nchi sijui wanaishi binadamu au....?
Najua unaumia sanaHii nchi sijui wanaishi binadamu au....?
Mradi tu siku zinaenda.Najua unaumia sana
Kwa nini kusubiri kurenegotiate wakati mnaweza kujadili na kuona mapungufu na kurekebisha kama mikataba hiyo itapelekwa Bungeni kabla ya kusaini?Someni miswada vzuri....soma section II 5.2 & 5.3....inaipa mamlaka bunge kuiagiza serikali ku renogotiate makubalino waliyoyafanya na muwekezaji
Hivi wabunge wa CCM unawajua au unawasikia?Kwani lengo la wao kwenda si ni pamoja na kutoa maoni kuwa IJADILIWE KABLA YA KUSAINIWA? au wamesema maoni ya aina hiyo hayaruhusiwi?