Dodoma kumejaa,viwanja vya bunge vimefurika.Asasi mbalimbali za kiraia zimefika kutoa maoni yao juu ya miswaada ya dharula iliyoletwa mbele ya kikao cha bunge.TLS ya kina Tundu Lissu haijabaki nyuma,imetuma vijana machachali waliojipa muda kuchambua miswaada hii kwa uweledi mkubwa na kuibua mambo mengi sana ambayo "raia wa kawaida" anaweza asiyaelewe sababu ya kukosa uelewa wa sheria.
Licha ya uzuri wa sababu ya kuleta harakaharaka kwa miswaada hiyo,lakini bado vijana wa TLS wametueeleza kuwa moja ya mapungufu ya miswaada hii,ni kuwa serikali imeweka sheria kuwa mikataba yote ya madini itatakiwa kuletwa bungeni na kujadiliwa,lakini kuletwa kwake bungeni si kabla ya kusainiwa na serikali na wawekezaji,bali baada ya kuwa umeshasainiwa na wadau hao wawili.
Swali linakuja,kuna umuhimu gani au ulazima gani kwa mikataba ya madini,kupelekwa bungeni wakati ikiwa imekwashasainiwa?Kupeleka mkataba uliokwishasiniwa bungeni ili wabunge waujadili,inabadili nini kwa maendeleo ya nchi na mustakhabali wa faida ya rasimali ya madini kwa Taifa?
Hali hii imezua mjadala mkubwa sana,kiasi kwamba watu wengi wamezidi kusema hakukuwa na ulazima kutoa siku chache za kujadili na kutoa maependekezo.Lakini hili la kupeleka mikataba bungeni baada ya kuwa imesainiwa,lina faida gani hasa katika kipindi hiki tunacholalamika kuwa mikataba mingi tumeibiwa??