Wana JF,
Nilikuwa nafuatilia kwa makini mjadara wa kunyimwa fedha za wamarekani katika kutokomeza umaskini nchini, hali inaelekea kuwa ngumu muno hasa kutokana na taifa letu lililozoea utegemezi kuendelea kuziwaza hizi fedha wakati walengwa wenyewe zilikuwa haziwafikii kutokana na serikali kujipangia matumizi makubwa sana kuzidi uwezo wake, Aidha na serikali kutaka kupaa kiuchumi kujilinganisha na nchi kama Kenya wakati kenya walituwahi sana kielimu kwa kujifunza neno uzalendo , yaani kuipenda nchi yako popote, Wale vilizi wote wa fedha hizi potevu ndio wanaoshadadia pesa zilizofichwa Ulaya ambazo hazifanyi kazi yoyote.
Turudi kwenye point, watanzania wengi kwa sasa wanaendesha maisha kichina china baada ya kukosa ajira kwa muda mrefu, kwani serikali imeajiri watu hawazidi laki saba (sina takwimu) . wachina walipofika nchini, walikuta Tanzania imejaa fursa nyingi sana ambazo wanaweza kuzitumia wakapata ujira wao. Nchi ya china kufuatana na kwamba haina uwezo wa kuwaajiri wananchi wake , iliamua kufungua vyuo vingi vya ufundi wa kila aiana, Ufundi Ujenzi, Ufundi Chuma, Ufundi Nguo, Ufundi simu, Ufundi Redio. Wachina wakatambaa kila sehemu ya nchi mabli mbali kutafuta fursa, wakukutana na nchi ya Tanzania ambayo ina mkataba wa kimaneno kuwa ni marafiki wakaanza kujifunza kishwahili na kuungana kukamilisha urafiki.
Tukumbuke kwamba baada ya serikali yetu kututupa sisi ambao hatuna ajira, wachian wametengeneza ajira zifuatazo.
1.wamefundisha watanzania kutengeneza urembo kwa kuchonga vitu mbalimbali vinavyotumia chuma,.
2. wamewafundisha watanzania jinsi ya kupunguza taka taka kama plastiki na kuunda kitu kingine, mfano makopo ya plastik chakavu, yanatoa beseni, viti vya kukalia.
3. Wamefundisha watanzania biashara, ukienda kariakoo unaona jinsi wanavyomuangaikia mteja yaani wanakuvutia mpaka unanunua.
4. wamekusanya chuma chakavu yote na kuifanya Nondo, leo hii nchi yetu haizalishi chuma cha kutosha sijui ingekuwaje.
5. wamefungua milango ya kuingia nchini mwao kama kwao, vijana wamejifunza biashara, leo hii kariakoo, mwanza, na arusha ni tegemeo la nchi za jirani kuja kuemea product za kichina zinazotengenezwa tanzania.
Tufike hatua tukubali kuwa heri ya nchina kuliko mzungu, mhindi. kama ni suala la wageni mbona hapa kuna warundi kibao hadi mnawapa uraia wakati hawa tija, kuna wakenya, waganda hata matapeli wa Nigeria lakini bado wanakumbatiwa.
achina njjoni kwa wingi mtufundishe kulima,kuchonga vinyago, kutengeneza viwanda vidogo vya kuzalisha wembe na sindano, hata viwanda vya gongo ambayo imepimwa kwa viwango nasi tukapoze umaskini, maana TBL kila kukicha ni kupandisha bia tu.