Kemikali ya Zebaki ni nini?
Kwa mujibu wa taarifa zinazopatikana Mtandaoni, Zebaki ipo katika metali ya kimiminika na inapoingia kwenye mwili inakaa kwa muda marefu na kusababisha madhara kiafya.
Huathiri mifumo ya fahamu na kupata madhara ya msongo wa mawazo, kupoteza usikivu, uono na wengine kupata hali ya kutetemeka, kuathirika kwa moyo hata figo.
Pia Matumizi mabaya ya kemikali hizo ni hatari kwa afya, kwani madhara hayataonekana haraka lakini baada ya miaka 10 ndipo yatakapoanza kuonekana ikiwemo kutetemeka mikono, miguu na kichwa, ngozi kubabuka, saratani, figo, moyo mimba kutoka, watoto kuzaliwa na utindio wa ubongo na kuchanganyikiwa na hata kifo.
Imeelezwa wachimbaji wengi wanatumia kemikali hiyo bila kuchukua tahadhari zozote za kiusalama kama vile kuvaa mavazi yanayowakinga kugusana na kemikali hiyo, kuvaa glove mikononi, barakoa na mabuti na hivyo kujikuta wanaathirika na kemikali hiyo baada ya kipindi cha muda mrefu.
Mgodi wa Buzwagi katika Wilaya ya Kahama
Mgodi wa Mwakitolyo namba 5 uliopo Wilaya ya Shinyanga
Mgodi wa Buhemba Wilayani Butiama Mkoani Mara
Mgodi wa Njawale ulipo Wilaya ya Luangwa mkoani Lindi
Maoni ya Wachimbaji niliozungumza nao
01 - Mmoja wa wachimbaji wadogo aliyejulikana kwa jina moja tu la Alex ameeleza yeye alipata ulemavu wa ngozi kutokana na kufanya kazi hiyo kwa muda wa Miaka 10 sasa, kwa muda mrefu ametumia zebaki na sasa imemuathiri japo mwanzo hakufahamu chanzo cha tatizo lake mpaka alipoenda kupima.
02 - MamaTarifa amesema amefanya kazi hiyo zaidi ya miaka 12 sasa, hakujua madhara ya kemikali mpaka pale alipopewa elimu hiyo japo anaona madhara yalishampata makubwa lakini hawezi kuacha kuitumia kutokana na shughuli ya uchimbaji madini ndio ambayo anaitegemea katika uendeshaji familia yake, kwani imemsaidia kusomesha watoto wake na Kuanzisha miradi mbalimbali
03 - Mchimbaji aliyefahamika kwa jina moja tu la Michael amesema wakiwa maeneo hayo ya machimbo wanashuhudia wenzao wanaugua kwa muda mrefu hasa mapafu, moyo na wengine mpaka wanapoteza Maisha.
Pia anaeleza juu ya dhana potofu ya matumizi ya zebaki kwa baadhi ya wachimbaji kuinywa kemikali hiyo kwa lengo la kujipima kama ana ugonjwa wa vidonda ya tumbo ama laah.
Anasema ili kuthibitiaja hilo kama hana ugonjwa huo huwa wanakunywa endapo ikipitiliza tu wanajua hauna lakini kama ikibaki tumboni basi wanaamini imenasa tumboni na wanafikiria ya kwamba unakuwa na ugonjwa huo kwani kemikali hiyo ni nzito mno kwahiyo haiwezi kukaa tumboni kwahiyo anapomeza huwa wanaitoa kwa haja kubwa na wanapima kuwa alimeza gramu ngapi na imetoka gramu ngapi endapo kama ikitoka yote anahisi hana ugonjwa huo ila kama itabaki ana ugonjwa huo.
Ushauri wao kwa Serikali:
1_Mmoja wa wachimbaji anahisi kundi la wanawake elimu zaidi inahitaji kutokana wengi wao kuifanya kazi ili waendeshe maisha yao ndio waathirika Wakubwa kutokana na kuosha mchenjua mchanga wenye dhahabu kwa kutumia mikono bila uwepo wa tahadhari yoyote dhidi yao
2_Mmoja wa wachimbaji hao, alisema kutokana na ukosefu wa elimu juu ya matumizi salama ya kemikali ya zebaki inasababisha wengi wao kupata madhara ambayo hayana tiba kutokana na kufanya shughuli hizo bila kuchukua tahadhari yoyote vyema elimu itolewe
Ambapo elimu hiyo itasaidia kuondoa imani potofu hasa katika maeneo ha yo ya machimbo katika .masuala ya matumizi ya kemikali hiyo
3_amesema mbali serikali kutoa elimu stahiki juu ya madhara ya kemikalu hiyo lakini mpaka leo haoni kama kuna suluhisho la mbadala wake wa matumizi hayo ya kemikali jambo ambali linashangaza kutokana na changamoto kuendelea kuwa mkubwa miongoni mwao ambapo baadhi ya wachimbaji Wenzao kufariki kutoka na ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza Maisha.
4_Mchimbaji mwingine Charles Misalaba alisema yeye ni miongoni mwa waathirika wa kemikali ya zebaki, kwamba amekuwa mtu wa kupoteza kumbukumbu kuwa na hasira muda wote na kuwa na msongo wa mawazo.
Hivyo aliiomba serikali kuangalia namna ya kumsaidia kupata tiba yake ili kuondokana na adha hiyo.
5_Kutokana na Sekta hiyo kuajiri wananchi wengi mchanganyiko Me/Ke na wengi kutegemea shughuli hiyo kwaajili ya kuongeza kipato chao na serikali imetakiaa vyema mikakati ifanyike kwa lengo la kuwalinda kiafya wachimbaji ili iwe endelevu.
6_Serikali kuweka mikakati hai isiyokaa muda marefu ili kuawawezesha wachimbaji kuchukua tahadhali.
7_Wanajiuliza kwanini mikakati mingine inafanikiwa kama ya Magonjwa mbalimbali kama HIV lakini kwanini elimu hafanikiwi ya kupunguza matumizi ya kemikali hiyo ikiwa serikali inapata faida kupitia rasilimali hiyo.
8_Vifaa vya uchimbaji bado ni gharama sana na inayowafanya kutumia vifaa vya kienyeji ama wasitumie kabisa kwanini serikali isipungunze kodi katika vifaa vya kujikinga kama Gloves ili wahusika wawe salama katika shughuli ya uchimbaji na kupunguza waathirika.
9_ Ali Mohammed ameeleza mbali na kuelimishwa juu ya utumiaji wa kiasi wa zebaki lakini wanasema hakuna mbadala wake hali inayowafanya wachimbaji kuendelea kuitumia.
10_Vyema mkataba wa Minamata wenye lengo la kutekeleza mradi wa kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji ulete matokeo chanya ili wachimbaji waweze kuwa na mazingira yenye viwango vinavyohitajika kwa mujibu wa mkataba huo.
====================================
Hii ni stori iliyotolewa na NEMC, Novemba 5, 2024 walipotoa angalizo kuhusu matumizi ya ZEBAKIWITO WATOLEWA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI KUACHA MATUMIZI YA KEMIKALI YA ZEBAKI (MERCURY)
Wito watolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuacha matumizi ya kemikali ya zebaki (Mercury) na kutumia teknolojia mbadala kwenye uchenjuaji wa dhahabu ili kulinda afya ya binadamu na Mazingira.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi. Cyprian Luhemeja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kikanda wa Nchi za Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu (EHPMP), Mkutano unafanyika katika Hoteli ya Hyatti Regency jijini Dar es salaam.
Mhandisi Luhemeja amesema Mkutano huo umelenga majadiliano ya namna bora ya kuacha matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo, huku akitaja tani zaidi ya elfu 18 ya kemikali ya zebaki hutumika nchini Tanzania kwa mwaka hali inayohatarisha afya ya Viumbe hai na Mazingira.
“Lengo kuu la Kongamano hili ni kujadili namna bora ya kuondokana na matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo kwa sababu zebaki ni hatari kwa afya ya binadamu na Mazingira. Inakadiliwa kwa mwaka tunatumia kemikali ya zebaki zaidi ya tani elfu 18 ambapo sehemu kubwa ya watumiaji ni wachimbaji wadogo hivyo tunafanya juhudi ili kudhibiti matumizi ya kemikali ya zebaki” amesema Mhandisi. Cyprian Luhemeja
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema zebaki ni hatari kwa afya ya binadamu, vyanzo vya maji na mifumo mingine ya ikolojia, hivyo ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kutumia teknolojia mbadala za kisasa kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu.
Mkutano huo unakutanisha wadau kutoka nchi mbalimbali dunia zikiwemo nchi 5 zinazotekeleza Mradi huo ambazo ni Ghana, Kenya, Senegal, Zambia na Tanzania ambapo pia ni Nchi mwenyeji wa Mkutano.
Chanzo: Ofisi ya Makamu wa Rais