Elimu haina mwisho
Wabunge wetu ni watu makini na kama walivyoenda kujifunza kule Dubai na wakaja kufanya maamuzi yenye maslahi kwenye uwekezaji wa bandari,
Tunawaomba wabunge wetu hata 100 wakiongozwa na spika waende na kile chombo cha Ocean Gate chini ya bahari ili walete mrejesho wa meli ya titanic na waone namna ya kushauri mambo ya utalii wetu na jinsi ya kuukuza,
Kwa sababu tuna bahari hiyo itachochea utalii wa baharini,
Wabunge wetu kama msukuma na Lusinde wajumuishwe humo,
Lakini pia ili kupata ripoti nzuri watangazaji wetu nguli kama kitenge, hando na zembwela nao waende ili kurekodi habari kamili na celebraties wetu kama Baba levo, mwinjaku, steve nyerere waende kuwakilisha kundi la wasanii,
Dunia ni kujifunza kama walivojifunza dubai waende pia huko wakajifunze mambo ya utalii,