Wabunge wetu wamelewa vyama

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,423
13,935
Bunge, mbunge na ubunge ndio alama kuu ya demokrasia kwenye taifa lolote. Bunge imara litazaa serikali na mahakama/sheria imara pia.

Bunge letu sio kabisa, wanachojali wao ni vyama vyao tu vinasema na kutaka nini kifanyike. Siku watajikuta hata nafasi na hadhi yao ndani ya wanajamii ikiporomoka kidogokidogo, polepole na hadi kupotea kabisa, kuna siku itaonekana hakuna haja ya kuwepo wabunge. Mfano, yule mbunge wa wakati wa Adam Sapi Mkwawa, Pius Msekwa, Samuel Sitta, Anne Makinda, na Job Ndugai ni tofauti kabisa kwenye jamii. Ukiulizia kwanini inakuwa hivi utaambiwa vyama wanakotoka ndio sababu kubwa. Wanashindwa kusema NDIYO kwenye jambo linalowapasa waseme NDIYO hata kama ni zuri namna gani, pia wanashindwa kusema HAPANA kwenye jambo linalowapasa kusema HAPANA. Dhami hii itawatafuna wao kwanza kama wabunge kisha taifa. Iko siku watu fulani mwaka fulani watakuja kubana matumizi kwa kuondoa nafasi na kazi za wabunge, madiwani na mameya nchini.

Wabunge waache kuangalia vyama vyao, bali waliangalie taifa linakoelekea kama wao wakiendelea kutotimiza majuku yao kikamilifu..........!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…