Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 61
- 162
Tundu Lissu, akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa Clubhouse mnamo Desemba 23, 2024, alieleza kuwa endapo atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, ataweka ukomo wa ubunge wa viti maalum. Lissu alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wanawake wengi wanaokipigania chama wanapata fursa ya uwakilishi badala ya nafasi hizo kuwa miliki ya kikundi kilekile cha watu kwa miaka mingi
Binafsi, nakubaliana na hoja ya Lissu. Hata hivyo, ningetamani nafasi za viti maalum ziondolewe kabisa. Sababu kubwa ni kwamba wanawake wa sasa wana uwezo mkubwa wa kushiriki katika siasa na uongozi mbalimbali. Hivi sasa Tanzania tuna Rais mwanamke, Spika mwanamke, na mawaziri wengi wanawake, hali ambayo ilikuwa tofauti na zamani.
Wabunge wa viti maalum watemwe ili
Wabunge wa viti maalum wengi wanakosa ubora wa kiutendaji kwa sababu hawajapitia mchujo mkali. Mara nyingi hujikuta wamebweteka bungeni na hawatoi michango ya maana. Kuwapa nafasi wengine kutaleta sauti mpya na mawazo tofauti, jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Wabunge wa viti maalum wanaweza kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi au makundi maalum wanayoyawakilisha zaidi ya kuwajibika kwa vyama vyao vya siasa vilivyowapa ulaji. Mabadiliko ya mara kwa mara yanaweza kuongeza uwajibikaji kwa kuhakikisha kuwa wanapimwa kwa utendaji wao kabla ya kuteuliwa tena.
Kama alivyoeleza King Musukuma, wabunge wengi hupata msongo wa mawazo na hata kufilisika kutokana na kutumia kiinua mgongo chao kutoa rushwa ili kuchaguliwa tena. Hali hii pia inahusisha wabunge wa viti maalum, ambao hutumia nafasi zao kuhonga wajumbe.
Upendeleo katika uteuzi wa wabunge wa viti maalum pia ni tatizo, ambapo nafasi hizo mara nyingine hupewa watu wenye uhusiano wa kifamilia au wa karibu na viongozi wa vyama kama ilivyokuwa kwa Joyce Mukya ambaye ni mzazi mwenza wa Mbowe.
Wabunge wa viti maalum mara nyingi wanakuwa tegemezi wa nafasi hizo kwa miaka mingi, wakihofia kujaribu kushindana katika nafasi za ubunge wa majimbo. Miaka mitano ya viti maalum inapaswa kutosha kuwaandaa wanawake kupambania nafasi za ushindani moja kwa moja.
Ni hayo tu.