Najua sasa hivi huko kwenu kuna ukavu kama ule wa ukavu macho, na mnapo angalia kwa kupitia dirishani mnaona rangi nzuri ya kijani kibichi kilicho stawi vizuri kutokana na neema ya wakazi wake, licha ya mvua kunyesha lakini bado bara ardhi yake ukitupa ndala chini inarusha vumbi na hii inatokana na wakazi wake kukosa neema inayosababishwa na uovu wa mioyo yao, si ajabu ukipita njiani ukakuta mchunga ng'ombe kafa njaa na ng'ombe zake na ndio maana ukikaa boda nyuma ya rufiji utakuta ng'ombe zikiingia toka bara zikija pwani. Msitumie silaha kuja pwani sisi hatuwezi kupigana bali sisi twahitaji pesa maeneo yapo mazuri na tambalale.
Pwani ndio mahala pekee palipo bakia Tanzania na misitu, na kama tukiipoteza basi Tanzania yote itakuwa kavu.