Kwa ufupi
Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo, Agnes Mhina alisema upande wa mashtaka umethibitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka kuwa Juma Omari (30) na Samwel Shoo (23) walitenda kosa hilo.
By Hussein Nyari, Mwananchi
mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Hai. Mahakama ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, imewahukumu kifungo cha maisha jela wakazi wawili wa mji wa Bomang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne.
Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo, Agnes Mhina alisema upande wa mashtaka umethibitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka kuwa Juma Omari (30) na Samwel Shoo (23) walitenda kosa hilo.
Hakimu Mhina alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka, umethibitisha kuwa washtakiwa walikabidhiwa mtoto huyo ili wamrudishe nyumbani kwao eneo la Kengereka.
Ilidaiwa Juni 20,2015, mshtakiwa wa kwanza Juma, ambaye ni dereva wa bajaji, alikabidhiwa mtoto huyo badala ya kumfikisha alikoelekezwa, akashirikiana na Samwel kumbaka.
“Adhabu ya kosa mlilolifanya ni kutumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwenu na wengine wenye tabia kama zenu. Haya ni matukio mabaya na yanazidi kuongezeka nchini,” alisema Hakimu. chanzo.
Wabakaji wahukumiwa maisha gerezani