Waandishi wa Kikenya na Kiswahili kibovu BBC

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
63,595
89,120
Moise Katumbi: Serikali ya DRC ilijaribu kuniua
  • Saa 2 zilizopita
Mshirikishe mwenzako

Image copyright
Image caption Moise Katumbi: Serikali ya DRC ilijaribu kuniua
Kiongozi wa upinzani nchini DRC ambaye pia ni mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi ujao amesema kuwa serikali ya rais Joseph kabila ilimpa sumu katika njama ya kumuua.

Mwanasiasa Moise Katumbi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo anasema kuwa alidungwa sindano iliyokuwa na sumu nje ya mahakama ya Lubumbashi mnamo mwezi Mei.

Katumbi anasema haikujulikana sindano hiyo ilikuwa na nini.

Hata hivyo anasema askari polisi mmoja alimdunga sindano katika mshikemshike nje ya mahakama polisi walipofyatua mabomu ya kutoa machozi kwa mashabiki wake alipokuwa akienda kujibu mashtaka ya kuwaajiri mamluki kuwa walinzi wake kinyume cha sheria.

Bw Katumbi anasema kuwa madai hayo dhidi yake ni ya ''upuuzi''.


Image copyright AFP
Image caption Mwanasiasa Moise Katumbi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo anasema kuwa alidungwa sindano iliyokuwa na sumu nje ya mahakama ya Lubumbashi mnamo mwezi Mei.
Hata hivyo kiongozi huyo ambaye ni mkurugenzi mkuu wa klabu ya TP Mazembe aligonjeka na akalazimika kukimbilia nje ya nchi ilikupata matibabu.

Katumbi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa alikwenda Afrika Kusini Uingereza na kisha Ujerumani kutafuta tiba.

Waziri wa mawasiliano bwana Lambert Mende hakujibu mawasiliano dhidi ya serikali yake lakini kwa siku nyingi amepuuzilia mbali tuhuma kuwa polisi wa DRC walimdhuru bwana Katumbi.

Naomba kuuliza
Aligonjeka ndo nini? na je neno hili lipo kwenye Kamusi? Na ni Kiswahili sanifu? Ifike wakati tutoe malalamiko juu ya Kiswahili kuingiliwa na lugha zisizo rasmi!


nomasana, sam999, NairobiWalker, hbuyosh, msemakweli, simplemind, Kimweri, Bulldog, MK254, Kafrican,Ngongo, Ab_Titchaz,mtanganyika mpya, JokaKuu, Ngongo, Askari Kanzu, Dhuks, Yule-Msee, waltham, Mzee, mombasite gabriel, Juakali1980 , Boda254, mwaswast, MwendaOmo, Mwanakijiji, Iconoclastes, oneflash, Kambalanick, 1 Africa, saadeque, burukenge, nyangau mkenya, Teen-Upperhill Nairobi, kadoda11
 
Aligonjeka yamaanisha aliugua, kama unafikiria lahaja yako ndiyo hati miliki ya kiswahili rauka kutoka kwa ndoto.
 
Ngoja niende kwenye kabati langu la vitabu nikatafute kamusi yangu nitarudi!
 
Aligonjeka yamaanisha aliugua, kama unafikiria lahaja yako ndiyo hati miliki ya kiswahili rauka kutoka kwa ndoto.
neno hilo halipo kwenye Kamusi iliyopitishwa na baraza la Kiswahili Afrika Mashariki kwa hiyo halipaswi kutumiwa katika BBC Kiswahili! Hiyo ni shengi na ndo maana nimewaandikia kuwalalamikia BBC Kiswahili naomba nawe ufanye hivyo kukilinda Kiswahili!
 
Kudadadeki haipo, najua dogo std 7 kaichukua maana siioni. Ngoja nikaichukue maana siwezi kuchangia hadi niwe na egemeo(reference)
 
neno hilo halipo kwenye Kamusi iliyopitishwa na baraza la Kiswahili Afrika Mashariki kwa hiyo halipaswi kutumiwa katika BBC Kiswahili! Hiyo ni shengi na ndo maana nimewaandikia kuwalalamikia BBC Kiswahili naomba nawe ufanye hivyo kukilinda Kiswahili!
Ngojea toleo lijalo
 
BBC swaili sikuizi imekua uchwara sana aina hata mvuto tena wanakopi tu
 
wakenya wameingiza ukabila wanaajiri watu wasio na sifa! Nimelalamika juu ya hili!
kwahivyo hivi unadai BBC , imewachia bbc easy afrika iongozwe na wakenya bila uamuzi wowote kutoka UK, kana kwamba ni kituo cha kenya????
acha zako wewe, bbc inawakilisha mambo ya nje (foregn policy) ya waingereza, hawawezi achia kila kitu kwa nchi nyengine, lazma wafwate malengo ya bbc hq
 
ukweli ni kwamba waandishi wenu hawana vigezo wanaharibu Kiswahili!
 
Kuna kipindi hawa wakenya
Walilalamikia Watangazaji kutoka Tanzania kuwa wengi BBC Swahili
 
ukweli ni kwamba waandishi wenu hawana vigezo wanaharibu Kiswahili!
skiza hii basi

wakenya kadri hawajawahi kugonjeka na ugonjwa kama huu unaoitwa kiswahili sanifu, lakini wengine wao hukosea kosea maana si lugha yao ya kwanza kwani hao si wa bantu
 
nimetumia gonjeka vizuri sana hapo, lazma hio gonjeka ni kiswahili sawa
 
skiza hii basi

wakenya kadri hawajawahi kugonjeka na ugonjwa kama huu unaoitwa kiswahili sanifu, lakini wengine wao hukosea kosea maana si lugha yao ya kwanza kwani hao si wa bantu
Umemaanisha nini hapa? Au ndo nyienyie nawaongelea hapa? kuna maneono kama kuugua au kuumwa au kupatwa na maradhi/ugonjwa! Hamna neno kugonjeka! stop trolling me! Instead u should b sayin' a word about this!
 
Umemaanisha nini hapa? Au ndo nyienyie nawaongelea hapa? kuna maneono kama kuugua au kuumwa au kupatwa na maradhi/ugonjwa! Hamna neno kugonjeka! stop trolling me! Instead u should b sayin' a word about this!
sasa kiswahili na dili za pipeline zinashikana na wapi ? we umekosa kazi...

kama kiswahili kimeswahilisha maneno kama Konsonanti (hahaha), na kama wabongo wanatumia maneno kama endaga, basi pia sisi tutarahisisha mazungumzo na maneno kama gonjeka, kumbuka gonjeka ni ile hali ya kupatwa na ugonjwa kwahivyo hauzi ukasema kuugua au kuumwa. unaeza sema kupatwa na maradhi lakini kumbuka sisi huku wengi wetu hupenda kutumia sentensi fupifupi na kufanya 'small talk' kwahivyo siezi anza kusema ,'alipatwa na maradhi' wakati naeza sema aligonjeka
...(hapa tumetumia gonjeka kama kitenzi kumaanisha ile hali ya kupatwa na maradhi)
kama hautaki neno gonjeka, basi hili neno lengine ambalo limefanana na gonjeka nalitumia kwa sentensi

nomino dhahania ni nomino ya vitu ambavyo tunavitambua kwa macho,harufu nk, yani vitu ambavyo haviwezi gusika wala KUONJEKA




u
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…