Inatisha sana pale ambapo biashara haramu zinakuwa ni tamaduni za jamii ya watu fulani.
Kuzimaliza itakuhitaji upige Vita dhidi ya serikali, wafanya hiyo biashara na raia wa kawaida ambao kwa namna moja au nyingine Uchumi wao halali unakuwa umeunganishwa na Uchumi haramu.
Sawa na leo mtu aseme anaanzisha Vita dhidi ya biashara haramu kwenye nchi kama Italy au Mexico. (Haiwezekani hata kidogo)
Lazima tu Uchumi utaanguka kwasababu Legal Economy (Uchumi Halali) umeunganishwa na Uchumi haramu (Underground Economy). Nchi kama Mexico biashara haramu ya Madawa ya Kulevya ndiyo imejenga mashule, barabara, viwanda na kuajiri vijana wengi haramu: mpaka walipofika sasa hata serikali haiwezi kupigana na wauza unga bila kujiumiza yenyewe sanjali na Uchumi wa nchi.
Tanzania yetu sasa ndiyo majanga matupu.
Uchumi haramu umekuwa unaendesha nchi kwa miaka miongo zaidi ya mitatu.
Ukwepaji kodi na utakatishaji wa pesa , Ujangili, Rushwa, Biashara ya binadamu, Madawa ya kulevya, Wizi wa madini , Uuzaji wa Silaha za moto n.k
Bahati mbaya sana wanaojihusisha na hizi kazi haramu ndiyo:
1. Wawekezaji wakubwa hapa nchini hivyo basi wao ndiyo watoa ajira wakuu.
2. Wanasiasa wetu. (wengine wameshika hadi nyadhifa kubwa kabisa na wengine ndiyo wapinzani wetu)
3. Wauzaji na wasambazaji wakubwa wa bidhaa muhimu kama Sukari, Mafuta, Nguo, Vipodozi, Nafaka n.k
4. Wamiliki wakubwa wa vyombo vya habari vyenye ushawishi hapa nchini.(Magazeti, Redio na Televisheni)
5. Wachangiaji wakubwa wa shughuli za Vyama vikuu vya siasa hapa nchini.
6. Wachangiaji wazuri wa shughuli za kijamii. (Wanajenga Makanisa, Misikiti, Zahanati, na Shule)
Ukiisha yaangalia haya basi utajua kwamba huwezi kuwashinda hawa mabwana bila kuumiza maisha ya Mtanzania wa kawaida. Hata leo angefufuka Hayati Mwalimu Julius Nyerere angeshindwa kuongoza nchi ambayo imejenga Uchumi ulio imara kupitia biashara haramu. Watanzania wenyewe wangempindua hata mwezi haufiki, kama tu miaka ya 80 wafanya baishara haramu walikuwa ni wachache lakini walifanya watakavyo Usitegeme leo ambapo wana magenge makubwa utaweza kuwashinda kirahisi.
I.M.F wametoa taarifa yao kwamba Uchumi harama (Underground Economy) kwa nchi zinazoendelea ni kama Asilimia 25% hadi 40% ya G.D.P za nchi hizo. Sasa fikiria Tanzania yetu ni moja ya nchi inayosifika kuwa mlango mkuu wa biashara haramu hapa duniani, sehemu kubwa ya Uchumi wa nchi ni baishara haramu. Sidhani kama serikali inaweza kushinda hii vita kirahisi hasa ukiangalia jinsi ilivyogawanyika kioungozi na kiutendaji kuanzia kwenye Ngazi ya Kitaifa hadi Ngazi ya Chama.
Ili nchi kama hii ifanikiwe na mabo yarudi kama kawaida inabidi nchi iongozwe na kiongozi ambaye ni Mafia Oriented ambaye ataendana na huu mfumo wa Kimafia. Mfano Mzuri ni Kenya na Nigeria, ambako Uchumi unakuwa kwa kasi lakini hauko mikononi mwa serikali bali Magenge ya Wahuni ambao ndiyo wenye kushikilia kila kona ya Uchumi wa nchi.
Good bye Afrika.
NB: Ni hat
EMT