Waalimu mnakera sana!

heavyload

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
918
525
Kwa bahati nzuri au mbaya nina watu wa karibu waalimu wengine shule za msingi wengine shule za sekondari.
Kwakweli nakereka sana juu ya tabia za waalimu makazini
Hawa watumishi hawapendani wao kwa wao,ni watu wa majungu kila siku,hawana ushirikiano,wamejawa wivu hata kifikia mahali pa kuoneana wivu wa mavazi
Wengine kujipendekeza kwa walimu wakuu na wakuu wa shule ilimradi tu mwingine aonekane hafai
Mitaani ndo usiseme dharau kwa wanakijiji hasa wakina dada / waalimu wa kike
Hii inanifanya niamini waalimu wa siku hizi hawana wito maana hata tabia zao si za kuigwa na ndio sababu walimu wengi wanaishia kula na kuvaa wengi wao maisha ni duni mpaka wanapostaafu na wakistaafu hawafanyi chochote cha maana kwakuwa na ushirikiano duni na jamii
Wito wangu kwenu waalimu badilikeni ili sekta ya ualimu iheshimike kwa kuanza kuiheshimisha wenyewe
 
nani kakwambia ualimu ni wito? hii ni kazi kama nyingine.


kuhusu majungu na kujipendekeza, hii ni tabia ya mwanadamu. hata bungeni unaona wabunge wanavyojipendekeza kwa mamlaka!

kuhusu ushirikiano miongoni mwao, sio lazima sana. urafiki haulazimishwi.


kujidai, hulka ya mtu, hata mpiga debe anajidai.


hitimisho:
walimu nawaomba mkaishi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi.
 
hayo yote yapo mkuu na watu wametoka sehem tofaut kubadilika n vigum sana cha endelea kuwaombea kama baba mkubwa anavyosemaga
 
Rusha mawe kwa Ngedere, Usisahau kujikuna upele, Yangu hayo tu!
Si walimu wote wapo hivyo lakini jaribu kutafakari, Ni hatua gani umechukua kuhakikisha unatatua hilo tatizo [Play your part kama mzazi au mdau wa elimu], Nami wito wangu Zungumza nao hao walimu wa Mahali Ulipo, na Ahsante ujumbe umefika kwa wengine.
 
Kwanza mtoa post post yako Ina matobo matobo mengi Sana Unaandika bila shaka unatoka kuzinduka baada ya kusurika na ajali ya mv bukoba mfyuuuuu
 
mengne yana ukwel ndan yake mana yanaonkana hata kwa macho huhtaj darubn mana haya watu kweny 18zao n htr sana yan kma vjjn mpka wanataman kuamukiwa na wazee wa kjjn hpo pnd wanawasnda umri
 
Dah hasa walimu wa kike mkuu one day niliazima bodaboda ya jamaa angu sasa madamu naye alitaka kwenda mjini ikabidi nimpakie.Asee nikimdunda kidogo kwenye korongo ananitusi dah nikimwangalia nimemzidi Elimu anaringa kweli ilibidi nivumilie kwa busara ila wakifika vijijini huko wanaona watu wote wajinga wao wajanja.Badae jamaa akamwambia umemtusi mtu usiyemjua ni nan aliishia kujilaumu tu.
 
Mtoa post povu limekutoka utakuwa kuna mwalimu umemtongoza kakukatalia
. achakuwadharau walimu. Kitendo cha kuwadharau walimu hakijawahi kumuacha mtu salama
Mkuu mimi sijawahi kufikiri kumtongoza mwalimu au ningetaka ningeisha fanya maana zipo njia nyingi za kumpata mwalimu kutokana kuwa wengi wao wana maisha magumu hatari
Kwa kifupi sina mahali naweza kutana na mwalimu maana ninapoweza kwenda kubarizi mwalimu hana uwezo wa kufika labda ajichange mwaka mzima.
Sanasana tunaonana wakifika niwakopeshe sukari 'unga na chumvi au nauli wakafuate mshahara vinginevyo kutokana na tabia zao sio wote sinaga mzuka nao
 
Kwa kifupi walimu wengi hawana nidhamu especially wakike wengine wakiume utawasikia unajua mimi nilikotoka maisha yetu sio duni!!!
Sasa si ungekataa post ya ualimu tukuone wa maana
 
Hapo sasa umekosea usikebehi hivyo mkuu hata kama wamekukosea sana hizo ni dharau acha mkuu hazita kusaidia chochote yote ya dunia mapito tu mbona matajiri kama kina baharesa hujawahi wasikia wakikebehi jifunze kwao mkuu usikute unatembea Toyota basi unakebehi watu hivyo ila anayetembelea hummer anawapa lifti wanyonge.
 
Mtoa post povu limekutoka utakuwa kuna mwalimu umemtongoza kakukatalia
. achakuwadharau walimu. Kitendo cha kuwadharau walimu hakijawahi kumuacha mtu salama
Serikali ya Tanzania imewadharau walimu tangu na tangu na hakuna lolote hebu acha mkwara.
 
Mtoa post umekosea tena sana kwa walimu" ungejaribu kuwasema waajiriwa wengine mf ,,,,,,,,,,,,,,,,,, ungepata wengi wa Ku share na ku like"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…