DOKEZO Vyuo wa Ualimu ngazi ya cheti bado vinaendelea na utapeli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

robbyr

Member
Apr 8, 2017
54
86
b6c0375ab30919a521bc39b3cc486ec3.jpg

[Picha: Wiki How]

Tupo kipindi ambacho wizara ya Elimu inapambana katika kuleta mabadiliko katika elimu hasa katika mafunzo ya walimu.

Ila kulinga na muongozo mpya ambao umetoka ili walimu waweze kufundisha ngazi ya shule za msingi lazima awe amehitimu kidato cha sita na kujiunga ngazi ya diploma mafunzo ya ualimu.

Lakini huku mtaani bado vyuo vinaendelea kudahili wanafunzi waliohitimu kidato cha nne.

Kitendo hichi naona ni utapeli na kuumiza wazazi na pia kupotozea muda vijana kusoma fani ambao pia hawatakuwa na vigezo katika kazi.

Hivyo naomba wadau na wizara husika waweke vigezo hivi ili vieleweke kwa wazazi na jamii ili kufikia malengo katika elimu yetu.

Asanteee
 
Back
Top Bottom