Vyuo vikuu Catholic Nchini Tz, vimezidi kuibana bodi ya mikopo kutoka na Serikali kupitia bodi hiyo kushindwa kulipa ada za wanafunzi ktk vyuo hivyo.
Mwishoni mwa mwezi wa 11 chuo kikuu Catholic-SAUT kiliazimia kutowahitimisha shahada mbalimbali wanafunzi zaidi ya 1000 baada ya kuidai bodi hiyo zaid ya 500 milioni kama ada, lakini baadae bodi hiyo ilijitokeza siku 2 baadae tarehe 29/11 kulipa deni hilo na hivyo wanafunzi hao kuhitimu shahada zao.
Chuo kikuu Catholic Cha Mwenge mjini Moshi-MWECAU, nacho kimeitangazia kiama bodi hiyo na wanafunzi wake katika mahafali yatakayofanyika tar 29/12 ambapo mwanafunzi anayelipiwa na bodi hiyo hatashiriki mahafali hayo labda alipe deni lake mwenyewe. Hayo yamewakumba wanafunz wengi wa sayansi chuoni hapo huku tukiitaja katika ndoto Tz ya viwanda.
Awali akihutubia maelfu ya Wahitimu katika Chuo kikuu cha SAUT- Mwanza tarehe 16&17/12 mbele ya Mkurugenzi wa Bodi hiyo Abdul Razzak Badru na Msemaji wa Bodi Bwana Cosmas Mwaisobwa aliyetunukiwa Shahada ya Uzamivu katika mawasiliano ya Umma katika chuo hicho, Makamu mkuu wa Chuo cha SAUT- MWANZA, aliishukuru bodi hiyo, kwa kulipa deni hilo na kuishauri serikali isiwe inawakopesha wanafunz masikini bali iwape msaada, kwani hawana uwezo wa kurejesha bali iwakopeshe watoto wa matajiri kwani dunian kote Maskini hakopesheki.