THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,922
- 13,494
Friends and Our Enemies,
Baada ya kuichukua Nchi katika kipindi kigumu zaidi cha kuondokewa na mtangulizi wake, kitu kikubwa alichokifanya ni kujenga IMANI.
Alijenga Imani kwa mfumo wa demokrasia kwa kuwahakikishia wapinzani kuwa haki itatendeka,na kwamba wote waliokimbia nchi mfano kama Lissu, Lema na kadhalika..warudi nchini tujenge nchi na hakuna yoyote wa kuwafanya lolote,na kweli wamerudi na kweli siasa wanafanya kama zamani.
Alijenga Imani kwa wafanya biashara kwa kuwahakikishia kuwa hakuna tena dhulma,hakuna kupokwa pesa zao,hakuna kubambikiwa kodi,na uhuru wa biashara utakuwepo kwao na hilo limefanikiwa.
Alihakikisha kuwa demokrasia ya kweli inarudi,vyama vya siasa viwe huru kufanya mikutano kama zamani na viwe huru kukosoa serikali pamoja na uhuru wa habari,hakuna tena mkono wa chuma...na hilo linaonekana leo.
Alihakikisha miradi yote ya kimaendeleo ambayo walianza pamoja na mtangulizi wake inaendelea na haiiishii nijani, na mingine mingi ianzishwe na iendelee.
Kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma na madaraja ambayo yalikaa kwa muda mrefu bila kuangaliwa wala kuzingatiwa,kuboresha hali za wakulima na kuhakikisha wanapata pembejeo zao za kilimo na mbolea kwa wakati na kuhakikisha bei za mazao yao kupitia stakabadhi ghalani zinaboreshwa na walanguzi wanaondolewa na hilo kafanikiwa.
2025 ni hii hapa kwenye kona,bila shaka wapinzani wake ndani ya chama kama wapo na nje ya chama pumzi zimekata kabisa,na hawaoni katika mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu Inshallah watatumia karata gani kumwangusha na kupata imani kwa wananchi.
Lakini kwa vyovyote vile iwavyo,hata kwa sasa bado yeye anaonekana kuwa ndie mwanasiasa maarufu zaidi na mwenye turufu ya kuaminika ndani ya chama chake na nje ya chama chake.
MUNGU AIBARIKI TANZANIA.