Mimi ni abiria ambaye natumia huduma ya Mwendokasi karibia kila siku hasa Kituo cha Kivukoni lakini kuna kero ambayo naona siwezi kuendelea kuifumbia macho.
Katika Kituo hicho huduma ya choo cha Abiria ndani ya kituo ni tabu tupu, kwanza vyoo ni vibovu, havitumiki, vinavyotumika ni vile ambavyo vipi nje ya Kituo ambavyo nivya kulipia.
Vyoo vya ndani ya Kituo hicho vimefungwa kutokana na kuharibika na havitumiki kabisa.
Kero kubwa ni kuwa hivyo vyoo vya nje vinaanza kutumika kuanzia Saa tatu Asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni wakati huduma za Mabasi zinaanza Alfajiri Saa kumi na moja hadi saa tano usiku.
Hiyo inamaanisha kuwa abiria au mfanyakazi akiwa na uhitaji Alfajiri analazimika kusubiri saa tatu asubuhi ndio apate huduma, pia yule ambaye atakuwa na uhitaji kuanzia saa moja usiku hadi tano usiku atalazimika kutafuta njia mbadala ya kutoa haja zake.
Hii hali inaweza kuonekana ya kawaida lakini ni jambo baya na linalotakiwa kuchukuliwa hatua haraka, suala la huduma ya choo ni muhimu kwa kila mtu. Kutokuwa na choo kunasababisha watu kuharibu mazingira.