Kumbe wenye vyeti ni wachapakazi?
Nilitegemea katika zoezi hili viongozi waandamizi serikalini hasa wa wilaya na mikoa wangelitafuta ufumbuzi kimya kimya kuliko kuanza kulalamika.
Malalamiko ya viongozi kuhusu huaba wa watumishi eti kwa sababu ya vyeti feki ni sawa na kupingana na Mh.Rais, wakati mwingine kunaonesha jinsi gani wakuu wa idara na taasisi za umma ambavyo hakujipanga kimkakati kukabiliana na upungufu wa watumishi.
Cha kufanya ni kuandika upya orodha ya watumishi waliokuwa na vyeti feki na kuonesha ni idara IPI,cheo gani ili kama kuna wenye nia ya kuomba nafasi hizo wafanye hivyo Mara moja.
Majina yameandikwa kwa ujumla sana,hakuna details za kutosha,hivyo kusababisha sintofahamu nyingi na wakati mwingine kuwaibua viongozi waandamizi kusema ni chochote.