SoC04 Vyama Vya Ushirika kwa Wafugaji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Rweyemamu Cleophace

New Member
Jun 4, 2024
3
1
Utangulizi: Takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya pili katika bara la Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikitanguliwa na Ethiopia,Hata hivyo pamoja na wingi huo wa mifugo lakini ufugaji wake mwingi umekuwa wa kienyeji, Sifa inakuwa kuwa na mifugo mingi lakini ufugaji huo siyo wa kitaalamu.

Jambo hili la kufuga bila utaalamu limewafanya wafugaji wengi washindwe kunufaika na ufugaji huo na pengine kuwakatisha tamaa kwa sababu wafugaji hawanufaiki na malighafi za mifugo kama maziwa, nyama, ngozi nk, Ufugaji wa kisasa na kitaalamu ungewafanya wafugaji waweze kuuza malighafi za mifugo nje ya nchi na kuwawezesha kupata kipato na kuliingizia Taifa pesa za kigeni.

SULUHISHO: Tanzania tuitakayo iunde vyama vya ushirika maalum kwa ajili ya wafugaji jambo ambalo litasababisha kuwaunganisha wafugaji na masoko makubwa ya malighafi za mifugo yao na kuwawezesha kuuza malighafi izo katika hoteli kubwa za nyota tano nk.

Ushirika pia utawasaidia wafugaji kuzalisha mifugo yenye ubora.Kama Taifa inatubidi tutoke kwenye ufugaji wa mifugo mingi usio na faida tuingie kwenye ufugaji wa mifugo wachache lakini wenye viwango vya kimataifa.

Faida za ushirika humuwezesha mfugaji kuwa na uhakika wa kuuza malighafi za mifugo, Mfano; Chama kinaweza kuwa kinapita kukusanya maziwa hata kwa mfugaji mwenye ng'ombe wawili au watatu na kuwatafutia soko.Vyama hivi pia vitawasaidia kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa ufugaji ili kuweza kupata mbinu na mawazo mapya ya ufugaji wa kisasa.

Serikali na Tanzania tuitakayo tunaomba ione faida za vyama vya ushirika lengo likiwa kuleta tija kwa wafugaji ili kuwatoa kwenye ufugaji wa kizamani lengo ni kuinua uchumi wa mwananchi mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom