Pamoja na uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani kisiwani Zanzibar kufanyika katika hali ya utulivu na amani , vyama vya upinzani vinavyoshiriki uchaguzi huo vimepinga uchaguzi huo kwa madai hauko huru na haki na una ukiukwaji wa sheria na katiba.
Hali hiyo inatokana na madai ya baadhi wagombea ya vyama hivyo ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha CUF ambavyo kwa nyakati tafauti wakiongea na ITV wamedai kutoridhiswa na utaratibu wa uchaguzi huo. Na wapinzani wamekuwa wakinyanyaswa kwa makusudi kwa madai ya kupiga baadhi ya wapiga kura.
Hata hivyo ITV imeshudia katika baadhi ya vituo wananchi wakijitokeza na kutumia haki yao ya kupiga kura bila ya hofu au uonevu ambapo jeshi la polisi likiwa limeweka ulinzi mkali kuhakikisha hakuna vurugu au fujo hali ambayo pia imeshudiwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohamed Mahmud akiwa na kamati nzima ya ulinzi na usalama na mgombea wa CCM Juma Ali Juma akipiga kura yake Fuoni.
Chanzo: ITV