Vyama vya Upinzani Tanzania vimejaa Wanasiasa wasiokuwa na Maono, Ubunifu wala uwezo wa Uongozi

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,723
5,374
Nje ya siasa za mikutano ya hadhara ya kupiga domo domo na maandamano ya kipuuzi puuzi vyama vya siasa vya upinzani Tanzania hakuna kitu kabisa! na hasa CHADEMA!

Na kwa kuwa Watanzania wengi ni watu wasiokuwa na elimu bora wala maarifa ya kuchanganua mambo kwa upana wake basi wanawafuata tu kama misukule Wanasiasa uchwara na mediocres na vyama uchwara visivyo na agenda wala mikakati yoyote ya maana ya kuwa mbadala wa CCM katika kuliongoza Taifa!

Mtu mwenye akili nzuri lazima ajue kwamba ili vyama hivi viwe na uwezo wa kuliongoza Taifa basi lazima vijenge mazingira ya ndani ya vyama vyao na nazingira ya nje ya vyama vyao ( yaani intra and inter political environment).

Mazingira ya ndani ya vyama ( intra political environment) ni lazima yavikuze vyama hivi kama taasisi imara za kiuongozi, tunapaswa kuona mifumo ya kiuongozi, demokrasia ndani ya Vyama, vyama kujijenga kiuchumi ( Miradi na Uwekezaji), miundombinu ya vyama ( kama vile najengo na vitendea kazi vingine n.k), njia bora za ufanyaji maamuzi ndani ya vyama! n.k.
Eneo hilo vyama vyetu hivi ni zero kabisa kidogo ACT WAZALENDO wanajitahidi!

Mazingira ya Nje (inter political environment) ya vyama ndio kama hivyo kupigania Katiba Mpya, Utawala wa Sheria, Mazingira sawia ya kufanyia siasa, kuitolea macho Chama tawala ( kwa sasa CCM), kuzungumzia rasilimali za Taifa n.k.

Huwezi kuitoa CCM madarakani kwa kupiga piga kelele tu majukwaani na maandamano ya kipuuzi puuzi tena kupitia Wanasiasa Uchwara wenye njaa tumboni na vichwani!

Jaribuni kujifunza kwa ANC ya Afrika kusini walivyojipanga kupigania ukombozi wa Afrika Kusini.

Akina Walter Sisulu, Oliver Tambo, Nelson Mandela, Giovan Mbeki ,Chris Han n.k walikuwa ni wanamikakati haswa!

Mojawapo ya mikakati walioweka ni pamoja na kujenga Uchumi wa Chama chao katika kuwawezesha kupambana na Makaburu!

Mpaka leo ANC ina vitega Uchumi Dar es Salaam (Tanzania), Lagos na Abuja (Nigeria) na kwingineko Duniani!

Leo miaka zaidi ya 30 ya kurejewa mfumo wa vyama vingi CHADEMA wameshindwa hata kujenga vyoo vyao achilia mbali Makao Makuu yenye hadhi ya Chama chao, halafu ndo waje na mdomo mdomo kuwa wanaweza kutatua changamoto za Watanzania!

Wajinga wasio na kazi za kufanya ndo wanajaza mikutano yenu! Penye ukweli tuambiane pasipo kubembelezana wala kuoneana aibu.
 
Haya wee siasa ni majengo na vyoo! Nipo jipya moja ambalo ccm wamefanya toka mkoloni pamoja na kukabithiwa dola! Kule PM mmoja amefumaniwa na mke wa mtu eti? Hayo mnayaweza sana!
 
Wenye akili msiowapuuzi mbona mnaogopa kuingia kwenye siasa?...jamii yetu inapaswa kubadilika. Waalimu tunapeleka waliofeli, wanasiasa hatutaki waliosoma-ilimradi ajue kusoma na kuandika. Polisi tunapeleka waliofeli form four, hatupeleki wenye div one au two...matokeo yake tunayaona.....
 
Andiko lako Lina kosa uhalisia kabisa kwani ccm Ina ajenda Gani mpya? Hiv katika Dunia ya sasa hivi Kuna chama kinaweza kikakosa ajenda? Na unalaumu vyama kukosa ubunifu mazingira ya siasa yetu hayakuruhu kuwa mbunifu na hata ukijaribu utaishia kusimangwa na kupewa majina mabaya .
Unaweza ukawa na mawazo mazuri nakukatilia kuwa vyama havina ajenda .
Kusema kuwa vyama vimekosa ajenda ni propaganda za ccm na wewe inaonyesha ni gamba tena ambaye unanufaika na ulaghai wa chama chako
 
Umeongea kwa kupanick mpaka imeonekana ni post ya shoga fulani. Kama ww ndio mpango mikakati ya CCM na ndio unaongea huu utoto, basi ujue hakuna chama hapo ndio maana mnategemea vyombo vya dola miaka yote.

Unasema CDM wameshindwa kujenga hata choo, hiyo ni kweli, lakini CCM pia hawana cha kujivunia maana 90% ya majengo yao ni ya kurithi toka mfumo wa chama kimoja. Na kuna mazingira mengi hayalipi kodi stahiki. Unasema ANC wanavitega uchumi hadi nje ya nchi yao, je CCM wanavitega uchumi wapi nje ya Tanzania?

Wanaokwenda kwenye mikutano ya CDM ni wasiojitambua na majobless, je wale wanaokwenda kwenye mikutano ya CCM wakati wa kazi wao wanashughuli gani? Acheni wivu wa kijinga nyie majizi ya kura. Ifahamike hata hao majobless wanaweza kupiga kura.
 
Ccm nao walewale tu imeiba mali za umma na kujimilikisha mf viwanja vya mpira na masoko,chadema wao ata jengo lenye hadhi hawana licha ya kuwa chama kikuu cha upinzani.ACT (hawa ni chawa wa ccm)hawana jipya zaidi ya kusifu Ccm,,Taabu tupu
 
Back
Top Bottom