Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,121
- 33,499
Kutokana na uhalisia wa kwamba Chama.Cha Mapinduzi kujikita kwenye siasa zenye malengo ya kuimaliza nchi ishindwe kuwa na uwezo wa kupata maendeleo ya kweli. Nimewaza sasa kutoa ushauri kwa vyama vya siasa hususani vya upinzani kuwapa mbinu za kufikia kutwaa dola kwenye chaguzi zijazo za serikali.
Natoa ushauri huu kama akiba kwani kuna uwezekano mkubwa leo nikaonhea hapa kwa uwazi kama alivyofanya Humphrey Polepole hapa juzi kati baafa ya kuwekwa kando na akili yake ikaanza kumrudia lakini kilichotokea ni kupewa ubalozi ambapo asali imemziba mdomo. Hivyo CCM haina wahuni tena wala viongozi siyo nyatunyatu kama alivyodai.... very shame. Serikali ina mkono mrefu inaweza kumsaka msanii kwa udi wa uvumba kisha ikamnyamazisha kwa njia tatu
CCM imejikita kwenye eneo la HADAA yaani uongo wenye ushawishi mwingi. Chama hiki kimehakikisha kuwa wananchi wa Tanzania hususan wanachama wake wengi wanakuwa wajinga ambao wanalishwa uongo mwingi kisha uongo huo wenye vimelea vya hofu unaenea ngazi ya familia hadi kwemye jamii.
CCM ni chama ambacho kilipokuwa no asset kilijikita kwenye siasa za ukombozi na kutetea wanyonge popote pale duniani ambapo kinaelewa mbinu karibia zote zinazotumiwa na wakandamizaji wa haki za binadamu. Viongozi wengi wa CCM ni zao la mfumo (ingawa tunaambiwa askari hawaruhusiwi siasa) hivyo ukifuatilia historia za wengi wesomea Urusi, Cuba, China na nchi ambazo zina ukandamizaji mkubwa wa haki za raia wake.
CCM imejikita kwenye kuhadaa kama nilivyosema awali. Wanaupiga mwingi sana kwenye hilo eneo. Hadaa yenyewe ni kuwa elites wachache wanapeana fursa za hatamu za nchi na wanahakikisha neno UDIKTETA linapigwa vita kwa nguvu zote lakini chama kama chama ni cha KIDIKTETA 100%.
Udikteta wa CCM umejikita kweye mbinu zote chafu tena zinazotishia amani ya nchi kwenye kushika Dola. Kuna muunganiko mkubwa kati ya mihimili yote ya Dola na Chama cha Mapinduzi kwenye kuhakikisha kinaendelea kuwepo madarakani huku kikiwa kimekufa kimeoza.
Kuna haja ya kuhakikisha jeneza la chama hili haliendelei kubebwa na Watanzania daima dumu. Zipo sababu 1001 za kuthibitisha CCM imefilisika kisiasa. Sababu nyingi zimeshasemwa na kuimbwa miaka yote hii na bado kimeendelea kukamata dola kwa kuwaibia wananchi Kura zao na kuwatishia ama kuwashughulikia wale wenye akili wanaojitambua na kuanza kudai UHURU wa kweli wa nchi hii
VYAMA VYA UPINZANI VIANZIE WAPI
1. SERIKALI ZA MITAA
Uchaguzi wa serikali za mitaa ni kipimo kikubwa kinachotumika kwenye kupima namna chama kinavyokubalika. Uchaguzi huo ambao miaka yote unafanyika kwa kiinimacho ni muhimu sana kwa vyama.vya siasa kuhakikisha vinafanya mikakati ya kupata ushindi mwingi. Viongozi wa serikali za Mitaa hukubalika kwenye jamii na kwa namma ambavyo madaraka yao yamejengeka wana ushawishi mkubwa na wanaweza kufanya mikutano ya kiserikali na kisiasa kwenye maeneo yao.
Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji na Kitongoji ndiyo wakuu wa Ulinzi na Usalama maeneo hayo. Hivyo dola inaheshimu mgawanyiko huo na hutumika sana kupin point wananchi ambao wanaonesha dalili za kuiumiza CCM kwenye uchaguzi wa serikali kuu.
Maeneo ambayo vyama vya upinzani vikapata ushindi mwingi wa serikali za mitaa hupelekea kupata washindi kwenye Uchaguzi Mkuu. Hata kura za urais kwa CCM zinapungua eneo hilo
2. NIDHAMU KWA CHAMA
Vyama.vya Upinzani wanapaswa kuweka mstari unaotenganisha majukumu ya chama na majukumu ya wanasiasa walioshinda chaguzi za serikali.
Usimamizi chanya kwenye eneo hili unapelekea kuibuliwa programu za kuwaandaa viongozi wenye weledi, nidhamu na mtazamo wa maendeleo jumuishi.
Vyama vya Upinzani vihakikishe vinatenganisha hizi nafasi ili kuwapa nafasi kila kiongozi kutimiza wajibu wake vizuri. Inapotokea kila anayeshinda uchaguzi wa serikali ndiye anayepewa chapuo kwenye uongozi wa chama hupelekea HADAA ya CCM kwa wananchi kupata dawati la kusikilizwa. Watasema vyama hivyo vina tamaa ya madaraka (ilhali CCM kina ulafi wa madaraka) na kina undugunaizesheni hivyo cha kibaguzi.
Viongozi wa vyama wajikite kukinadi chama, kuandaa ilani na kuzisimamia ilani zao kwenye maeneo waliyoshinda na kupokea taarifa za utendaji wa viongozi wao waliopo serikalini.
3. MAHUSIANO NA VYOMBO VYA DOLA
Ikumbukwe imesemwa sana hapa JF kuhusu ndoa isiyo ya kawaida kati ya vyombo vya usalama na CCM. Wengine walienda mbali zaidi kusema kuwa waajiriwa wote wa UT wana viapo vya siri vya kuitumikia TANU na ASP ambazo sasa ni CCM. Inawezekana kauli hizi zina ukweli kiasi fulani kwa sababu tunashuhudia UTII usio na afya kwa Taifa wa vyombo vyetu vya usalama kwa CCM.
Katiba ya Nchi imetenganisha askari na siasa lakini kwa sababu CCM ni nyakanga wa HADAA kinaishi kwa kutegemea mahusiano hayo.
Tukumbuke zile sauti ambazo zilisambaa mitandaoni za akina Nape, Kinana, Makamba na wemgineo zilipatikana kutokana na udukuzi uliofanywa na vyombo vyetu vya dola na wakazivujisha kwa umma ili kuhakikisha CCM inanufaika na umaluni huo. Chama cha siasa hawana access ya kuingilia mawasiliano ya watu bila usaidizi wa vyombo vya usalama wa nchi.
Hivyo vyama vya upinzani wakiona hakuna dalili ya kupata katiba mpya kabla ya Uchaguzi vijitahidi kupata kuungwa mkono na wananchi na vyombo vya dola. Haiyumkiniki wanao wanachama ambao pia wametokana na vyombo vya dola hivyo wakiwatumia hao wanaweza kuwa na mkakati wenye afya kwa Taifa
4. SERA ZA VYAMA
Nimevuka mstari wa mahaba kwa CCM. Ni bora mgonjwa akaondolewa mashine za kupumulia akalala kwa amani kwa sababu kuendelea kumhudumia hakutomfufua
Picha haihusiani na mada

- Kumtishia aache kuwananga CCM
- Kumpa nafasi kwenye sega la taifa
- Kumuita ziraili asepe naye

- Sera na Ilani vinapaswa kulenga kuwakomboa wananchi.
- Sera za vyama zijibu changamoto sugu zinazowakabili wananchi
- Vyama viweke tahadhari na mtazamo wa kijamii kwenye maoni yao kwa katiba na sheria mbalimbali zinazotungwa, vyama visikwame kwenye ibara ya 18 ya Katiba bali viwe na kurunzi la kumulika kila taabu na vijinasaba vya taabu vinavyowapa chanagamoto kwenye katiba na sheria..
- Theory of HITMAN isidhaniwe inatumiwa na mataifa yenye nguvu kouchumi dhidi ya madogo pekee. CCM imeadopt mbinu hii hivyo imepandikiza makada wake watiifu ndani ya vyama vya upinzani ili kuhakikisha wanavunja, kuharibu na kuua fikra zozote zenye maslahi ya kitaifa ambayo yanatishia UDIKTETA wake. Mfano wa kinachoendelea NCCR Mageuzi ni mwendelezo wa kuhakikisha vyama havitulii wala kujipanga kuingia kwenye chaguzi kwa utulivu.
- Demokrasia ya ndani ya vyama. Well hili kila mmoja anaelewa nini anapaswa kufanya ili kuonesha mfano wa nmna watakavyoishi kwenye dola endapo watapewa usukani wa nchi kupitia sanduku la kura endapo haki itatendeka.
- Vyama vifanye tathmini ya mara kwa mara kwenye kukubalika na kuelewea kwa wapigakura. CCM pamoja na kuwa ni nusu-kaputi wamejikita sana kwenye kutathmini kukubalika na kueleweka kwa chama na viongozi kwa wananchi. Tathmini hizi husaidia vikao vya maamuzi kwenye teuzi za kugombea nafasi za dola.
- Elimu ya Siasa. Vyama vya upinzani vianzishe darasa la kimkakati kila wilaya la kuwapika viongozi wake kisiasa na uelewa wa uendeshaji wa serikali. Viongozi wa CCM wanapitia semina mbalimbali za kujengwa na kupewa mikakati ya kuendelea kukamata dola. Mafunzo hayo hutolewa hata na watumishi wa umma (matumizi mabaya ya madaraka)
- Espionage kwa viongozi hususan mienendo yao kama inahatarisha dira ya Chama kwa maslahi ya umma. Hii pia isaidie kufanya maamuzi thabiti yenye tija kama CHADEMA kilivyofanya kwa wanachama wake 19 wa BAWACHA. Comcept kuu ni kulinda maslahi ya umma ambayo chama kinasimamia kwa mwelekeo waliojiwekea. Uwajibikaji uwe ni utamaduni utakaimarisha vyama hata kama wakiiga drama za CCM
- Vyama vipeleke mashushu wake CCM na kuwapenyeza ngazi za uongozi ili kwenda kuidhoofishana kufanikisha kuitoa madarakani kwa maslahi ya Tanzania. Mbinu ya TROJAN HORSE itumike kwa sababu vita vya kisiasa baina ya vyama na vyama imeasisiwa na CCM sasa ni wakati wa kuipelekea moto nayo pia.
- Vyama vya upinzani waimarishe misingi yao mashinani ambapo ndipo wapigakura walipo. Watumie ushawishi, weledi, hekima na busara kufanya shughuli zao huko chini. Hakina hilo litawaalika wenye misuli ya fikra ndani ya mfumo uliomilikiwa na CCM kuanza kuvijenga vyama hivyo kuanzia chini hadi juu.
- Vyama visiokoteze viongozi wanaotemwa kwenye michakato ya CCM kwa sababu inawezekana kabisa wametemwa kupitia drama ya kwenda kudhoofisha upinzani na hatimaye watarudi walipotokea kupeleka mrejesho na kadhalika