Kuelekea 2025 LGE2024 Vyama vya Siasa ongezeni uwakilishi wa Wanawake kwenye nafasi za uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
583
1,493
Wakuu nawasalimu.

Kama taifa tupo katika kipindi cha uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa ambao umepamba moto kwa hivi sasa. Huu ndio wakati wa Vyama vya Siasa nchini kukuza ushiriki wa wanawake katika siasa na maamuzi.

Vyama vya siasa vina jukumu muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia na kuhakikisha wanawake wanapata nafasi za uwakilishi kwenye uongozi. Kwa kuzingatia sera za usawa wa kijinsia, vyama vya siasa vinaweza kuhamasisha na kuwapa nafasi zaidi wanawake kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi kama wagombea na viongozi.

Kwa kuanzisha program maalum za mafunzo na uhamasishaji, vyama vinaweza kuwaandaa wanawake kuwa na ujasiri na uwezo wa kushiriki kikamilifu kwenye siasa. Hii itasaidia kupunguza pengo la uwakilishi wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi na nafasi za maamuzi.

Soma, Pia: Ni kwa namna gani Upendeleo wa Kijinsia huwakwamisha Wanawake kushiriki katika Siasa Tanzania?
Vyama vya siasa vinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuondoa vikwazo vya kijinsia na kuhakikisha wanawake wanashiriki kwa usawa katika maendeleo ya kisiasa ya nchi kwa kuwapa nafasi zaidi kuwania uongozi wa serikali za mitaa na vijiji.

Kwa mujibu wa kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania ilikua asilimia 2.1% ya wanawake wenyeviti wa vijiji, asilimia 6.7% ya wenyeviti wa vitongoji pamoja na asilimia 12% ya wenyeviti wa mitaa, hiyo ikiwa idadi ndogo ikilinganishwa na idadi ya vijiji na vitongoji vilivyopo nchini.

Soma: Kwanini wanawake huwa hawaoneshi nia ya kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za mitaa?
 
Punguza hasira mkuu,
Mawazo ya kikuda🚮 kama haya ya usawa wa kijinsia ndo yanapendwa na watawala ili mambo ya msingi kama Mabadiliko ya Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi, nk, yasipewe nafasi
Punguza hasira mkuu, jukwaa ni huru hili na wewe unaweza azisha uzi na tukakuunga mkono
 
Mleta mada ukitaka kujua huna hoja mtizame huyo aliyeokota dodo chini ya mnazi kwa kupata madaraka makubwa amefanya nini cha maana mpaka sasa.

Uongozi hauna huruma eti haki sawa hiyo haki sawa unayoitaka wewe walishajaribu ccm sasa ona msoto mkali tunaopitia leo.
 
Back
Top Bottom