Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 1,253
- 2,502
Kusema kuwa zaidi ya nusu ya vyama vya siasa nchini ni mapandikizi ni "gross understatement"! Nchi hii kuna chama kimoja cha upinzani; vingine vyote ama ni vyama vya mikobani vinavyowezeshwa na dola au vimerubuniwa na hiyo hiyo dola.Muungano wa vyama vya siasa hapa Tanzania ni kupotezeana muda. Ifahamike kuwa zaidi ya nusu ya vyama vya upinzani ni mapandikizi ya CCM. Na isitoshe kwa katiba hii hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Mbowe ajiandae.Kwa ufupi,
Kiongozi wasasa wa nchi hakubaliki popote Tanzania Bara, hakubaliki kwa makundi yote hasa wananchi wa kawaida(common people).
Anapondwa mno kwa kushindwa kuwa dereva Bora na mwenye msimamo. Wananchi wameshindwa kujua hasa falsafa yake ni ipi?
Wameshindwa kujua mwelekeo wa nchi ni upi? Lakini baya zaidi wanasema hana ubavu wa kupambana na ufisadi uliotamalaki nchi nzima. Hana power of command.
Hii ndiyo nafasi kwenu vyama shindani ya KUSHIKA DOLA, unganeni na wote muwe na mwelekeo mmoja
Amini, mtashinda na mtashinda asubuhi tu.
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Na hiki ndiyo wanakitumia Jamaa wa kijani kuwashinda nyie.
Hata mkoloni alitumia mbinu kama hii kuwatawala wa Afrika (devide and rule policy)
Wananchi Wana nia ya dhati ya kuwachagua lakini kuna mahala nanyi pia mnawachanganya,, wanashindwa kuelewa kama mnashindana na Magufuli au serikali ya sasa? Kidogo hii inatosha.
Unganeni 2025 wanaondoka Hawa,๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ
Muungano wa vyama vya siasa hapa Tanzania ni kupotezeana muda. Ifahamike kuwa zaidi ya nusu ya vyama vya upinzani ni mapandikizi ya CCM. Na isitoshe kwa katiba hii hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Ni kweli kabisa bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hata wakiunganisha vyama vyote vya Africa mashariki kwenye uchaguzi hawatatangazwa !! Suala sio kushinda bali ni kutangazwa !๐ ๐Watanzania na vyama vya siasa tunaungana kudai KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
Kuungana Kwa ajili ya Uchaguzi ni hatua ya pili.
Tuanze na RASIMU ya WARIOBA kwanza,
Tuanze na Tume HURU ya UCHAGUZI kwanza,
Baada ya hatua ya kwanza kukamilika ndipo tuendelee hatua ya pili.
Kabisa kabisa 101% Truth !Kilichotokea soko la Kariakoo kimenipa tafakuri
Watu wana malalamiko mengi sana ila pia hawana imani na Viongozi wote wa kisiasa na kijamii
Mgomo ule ungeitishwa na vyama vya Siasa usingefanikiwa kwa kuwa wengi hawana imani nao
hata pale Mnazi mmoja wale Wafanyabiashara walishapoteza imani na Viongozi wao ndio sababu hawakutaka kuchagua wawakilishi
Wawakilishi wasingeweza kutema nyongo kwa kiwango kile kama wangekuwa kwny 'closed door'
Taifa linakabiliwa na uhaba wa Viongozi wa kuaminika kwny Jamii, Kuanzia Serikalini, kwny shughuli za kijamii, kwny vyama vya Upinzani ba hata kwny nyumba za ibada
Viongozi ndani ya miaka hii 15-20 wamewatenda vibaya sana watu wao kiasi kwamba imani imepotea sana sana
hata ukiitishwa mchango kwny nyumba za ibada mtu anatoa mchango huku kiasi cha imani kwny matumizi ya ule mchango ni less than 50%