Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,153
- 3,089
Wakuu,
Hivi vyama vya upinzani vilikuwa wapi kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanza? Yaani Uchaguzi umeisha ndo wanaanza kutoa maoni?
Maoni haya yana umuhimu gani sasa hivi kama CCM wameshapora Uchaguzi na kushinda asilimia 99?
Naanza kuamini hivi vyama kweli ni CCM B
==============================
Vyama vitatu vya siasa vya ADA TADEA, NRA na UMD nchini Tanzania, vimependekeza mabadiliko ya mfumo wa usimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vikihimiza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) isimamie badala ya Ofisi ya Rais-Tamisemi.
Mapendekezo hayo yametolewa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na viongozi wa
vyama hivyo walipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wawakilishi wa vyama hivyo wamesema usimamizi wa uchaguzi na INEC utahakikisha uwazi, haki, na kuondoa mgongano wa maslahi uliopo kwa Tamisemi, ambayo pia inaratibu shughuli za Serikali.
Aidha, vyama hivyo vimeomba Bunge kuangalia namna ya kubadilisha sheria inayoipa mamlaka Tamisemi ili uchaguzi kama huo wa mwaka 2029 ufanyike chini ya tume.
Source: Mwananchi