Vurugu zisipewe nafasi uchaguzi Zanzibar

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MCHAKATO wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar unaendelea huku kukiwa na taarifa ya kuwepo viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani, pamoja na matukio ya makusudi yenye lengo la kuogofya wananchi ili wasishiriki kupiga kura za marudio muda utakapowadia.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ilikwishatangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Rais na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi, kutokana na kufutwa ule wa Oktoba 25, mwaka jana. Uchaguzi huo ulielezwa kufutwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuwepo kwa kasoro kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa ZEC, wananchi wa Zanzibar sasa watapiga kura Machi 20, mwaka huu kuchagua viongozi hao. Chama cha Wananchi (CUF) tayari kimekwishatangaza kutoshiriki ambapo Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad aliijulisha Tume hiyo ya Uchaguzi ya Zanzibar kuwa amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hatua iliyowafanya wanachama wa chama hicho nao kukataa kushiriki.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa tayari kuna vuguvugu lisilo jema visiwani humo kutokana na baadhi ya watu wasio na mapenzi mema na visiwa hivyo kutisha wenzao wanaoonekana kukubali kurudiwa kwa uchaguzi huo na kuthibitisha kushiriki.

Jambo hilo halikubaliki na linapaswa kudhibitiwa mapema na vyombo vya usalama vinavyohusika, ili uchaguzi huo wa marudio ufanyike kwa utulivu na amani. Hadi juzi vyama sita vya siasa vilikwishaithibitishia ZEC kuwa vitashiriki uchaguzi huo. Vilieleza sababu za kufanya hivyo kuwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo haki ya kidemokrasia ya kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza Zanzibar.

Vyama hivyo ni SAU, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Kijamii (CCK),Tanzania Labour (TLP), TADEA na Chama cha Wakulima (AFP). Katika maelezo yake yaliyonukuliwa na gazeti hili jana, Mgombea urais wa AFP kwenye uchaguzi huo, Said Soud alieleza juu ya kuzuka kwa hofu miongoni mwa wananchi kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani hasa katika kisiwa cha Pemba.

Kwa mujibu wa Soud, kuna watu wameanza kuwatisha wafuasi wa vyama vilivyothibitisha kushiriki uchaguzi huo, ili wasipige kura kwa kuweka alama ya X kwenye nyumba zao na kuwasambazia vipeperushi vyenye ujumbe unaoonesha kuwepo kwa nia ya kuvunja amani wakati wa uchaguzi huo.

Kutokana na maelezo yake, baadhi ya watu kisiwani Pemba wana msukumo wa kufanya vurugu kutokana na imani waliyojijengea kuwa uchaguzi visiwani humo hauwezi kufanyika bila CUF kushiriki, jambo analosema kuwa si la kweli.

Kutokana na hofu hiyo, mgombea huyo alisema kuwa aliamua kumuomba Rais John Magufuli kusaidia kuimarisha ulinzi katika eneo hilo kwa sababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, ili wenye kutaka kuuvuruga uchaguzi huo wasipate nafasi, kwa kuwa ndio njia pekee ya kidemokrasia inayoweza kuipa Zanzibar viongozi halali. Shime Watanzania wenzetu wa Zanzibar, msiruhusu uvunjifu wa amani
 
Kule Gwajima huku uchaguzi zanzibar du huyu M/kiti wenu kaleta shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiida.
 
Kwa ujumla hali si shwari sana pande hizi za unguja pia ,Watu wamekuwa katika sintofahamu kubwa na maisha yanazidi kuwa magumu kupita kiasi.Mahoteli mengi yameshapunguza wafanyakazi ingawa tunaelekea kwenye low season.TOFAUTI NA MIAKA YA NYUMA.HOTEL ZINAANZA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI MWEZI WA NNE WA KILA MWAKA.
 
Umezungumza kupiga kura ni haki ya kidemokrasia !demokrasia ni kwenda kupanga foleni na kupiga kura tu basi ,

Baada ya hapo hakuna tena demokrasia .maamuzi yanafanywa na jecha peke yake .lengo lenu ni kupeleka majeshi pemba .pemba kwa ustaarabu zaidi ya nchi yeyote duniani .mnatishwa na uovu wenu .huyu said suod hajawahi hata kupata diwani mara zote .kisa alipigwa na kijana mmoja wa cuf pemba n
Miaja mingi kwa sababu alikwenda pemba na kumtusi maalim seifu
 
1. Hizo alama za X zinawekwa na nani vile?
2. Amiri Mkuu wa Majeshi kesha sema sema ASIHUSISHWE na mambo ya Zanzibaa. Huo wito wa kupelekaAskari ni wa nini? Zanzibaa ni Nchi, ina vikosi vyake....
 
1. Hizo alama za X zinawekwa na nani vile?
2. Amiri Mkuu wa Majeshi kesha sema sema ASIHUSISHWE na mambo ya Zanzibaa. Huo wito wa kupelekaAskari ni wa nini? Zanzibaa ni Nchi, ina vikosi vyake....
Alisema kazi yake ni kulinda usalama ya nchi na watu wake ole wako ulete fyokofyoko utakiona cha moto.
 
Unaakili kama za matonya kabisa.
Kuna haja gani kusumbua watu wakati mshindi anajulikana?tuokoe gharama mkuu hizo pesa zisaidie kununua madawati na dawa hospitalini,huoni tutaokoa kiasi kikubwa kuliko zile za sherehe za uhuru?Nadhani Matonya umenielewa.
 
Kwani waangalizi wa kimataifa wataruhusiwa kuingia kutizama yatakayojiri Zanzibar
 
Alisema kazi yake ni kulinda usalama ya nchi na watu wake ole wako ulete fyokofyoko utakiona cha moto.
Ndugu yangu mie ni Mtanzania Mtiifu kwa viongozi wangu, hasa Raisi. Siwezi leta fyokofyoko yoyote. Kwanza ntaanzaje? Kwa sababu gani? Hapa Kamvini tunajengana kwa hoja na kuuliza hoja. Hii haimaanishi twataka kuleta fyokofyoko yoyote....Simiyu ni YETU pia.
 
Alisema kazi yake ni kulinda usalama ya nchi na watu wake ole wako ulete fyokofyoko utakiona cha moto.
Huyu dikteta ni muhim akafanya kama anavyofanya Nkurunzi burundi ...awauwe wapinzani ili amani itawale
 
Alisema kazi yake ni kulinda usalama ya nchi na watu wake ole wako ulete fyokofyoko utakiona cha moto.
Huu ubabe wenu nyinyi Chama Cha Majipu kwa kuamini vikosi vya ulinzi na usalama ndiyo vitaendelea kuwalinda na udhalimu wenu mkubwa wa kupora sauti ya wananchi waliyoifanya tarehe 25/10/2015 utakuja kusababisha madhara makubwa sana kwa nchi hii.

Hivi inawezekanaje huyo Magufuli adai kuwa hawezi kuingilia mambo ya Zanzibar, wakati akijua fika kuwa hata tangazo la Jecha kutangaza kuufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya marejeo ilitokana na 'kuamrishwa' na wahafidhina ndani ya chama chenu ambao huwa wanatamka waziwazi kuwa Zanzibar haiwezi kutolewa na vijikaratasi vya kupigia kura?

Kauli ya Magufuli ya kusema kuwa hawezi kuingilia uvunjifu wa waziwazi wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 uliofanywa na Jecha wa kufuta uchaguzi huo wakati hana mamlaka hayo na wakati huo huo akitamba kuwa yeyote huko Zanzibar atakayejitokeza mitaani na kupinga udhalimu mkubwa unaofanywa na CCM wa kuibaka demokrasia kuwa atatumia Uamiri Jeshi wake mkuu kutuma vikosi vya majeshi kuwadhibiti watu hao, hakika ni kama vile mkuu wetu wa nchi anataka kufanya 'booking' ili safari yake ya kwanza kabisa kwenda nje ya nchi aende ICC kuleThe Hague Uholanzi akajibu mashitaka ya ubakaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…