Vurugu zazuka tena uchaguzi BAWACHA, Polisi waingilia kati na watu kadhaa wakamatwa

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,509
3,992
Wakuu

Muktadha: Wakati mchakato wa kuhesabu kura kuwapata viongozi wapya wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) ukiendelea, baadhi ya wanaodaiwa kuwa makada wa chama hicho wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kuanzisha vurugu.
IMG_2565.jpeg

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa, Januari 17, 2025 wakati kura za wajumbe wa mkutano mkuu, baraza kuu, na viongozi wa Bawacha zikihesabiwa katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Soma: Vurugu zazuka nje ya ukumbi wa uchaguzi Bawacha, Wafuasi wa Lissu na Mbowe wazichapa

Inadaiwa wafuasi hao walianzisha vurugu wakitaka kuingia ndani ya uzio wa ukumbi huo, lakini hawakuruhusiwa kwa sababu si wahusika wa mkutano huo, hatua iliyozua mvutano kati yao na walinzi waliokuwa eneo hilo.
IMG_2566.jpeg

Mwananchi limeshuhudia askari polisi wapatao sita wakiingia kwenye korido za ukumbi huo kupitia mlango mwingine na kwenda moja kwa moja nje ya uzio wa ukumbi kuwakamata wanaodaiwa kuanzisha vurugu na kuondoka nao.



Vurugu zimeanzishwa na wanaume wanaodaiwa kurandaranda nje ya ukumbi walipo wapigakura.

Chanzo: Mwananchi

Soma, Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
 
😅😅😅, hawa watoto wakiambiwa waache mihemko hawasikii..

Ngoja wapelekwe jela kama Dr Slaa..
 
Mnachukua picha ya Mwaka juzi .

Mnaiedit kwakuiwekea Maneno Mwananchi, na Tarehe.

Ili ionekane ni habari ya Leo.


Hivi Lumumba hamna Vijana wenye Akili??.
 
Back
Top Bottom